T
Mandhari
Alfabeti ya Kilatini | |||||
---|---|---|---|---|---|
Aa | Bb | Cc | Dd | ||
Ee | Ff | Gg | Hh | Ii | Jj |
Kk | Ll | Mm | Nn | Oo | Pp |
Rr | Ss | Tt | Uu | Vv | |
Ww | Xx | Yy | Zz | ||
(Kwa matumizi ya Kiswahili) | |||||
ch | dh | gh | kh | ||
mb | mv | nd | ng | ng' | nj |
ny | nz | sh | th |
T ni herufi ya 20 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Tau ya alfabeti ya Kigiriki.
Maana za T
[hariri | hariri chanzo]- katika kemia T ni alama ya triti ambayo ni isotopi ya hidrojeni.
- katika ya fizikia "t" ni alama ya wakati (kut. tempus / time)
Historia ya T
[hariri | hariri chanzo]Kisemiti asilia T | Kifinisia T | Kietruski T | Kigiriki Tau |
---|---|---|---|
Tâw ilikuwa herufi ya mwisho katika alfabeti ua Wasemiti wa kale. Alama yake ilikuwa msalaba. Wagiriki walipopokea alama za Wafinisia waliiita alama Tau na kusukuma mstari wa kulala juu hadi mwanzo wa mstari wa kusimama.
Waetruski na Waroma wa Kale walipokea vile.