[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Wabenedikto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Benedikto wa Norcia, Mwanzilishi wa shirika

Shirika la Mtakatifu Benedikto (kwa Kilatini Ordo Sancti Benedicti au, kifupi, O.S.B.), ni utawa wa wamonaki wanaofuata Kanuni ya Mtakatifu Benedikto iliyoandikwa mwaka 534 na kuenea kote Ulaya Magharibi kama namna ya kawaida ya umonaki.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wabenedikto hawakubaki katika monasteri zao, wakishika maisha yao ya sala na kazi, bali walijitosa pia kueneza Injili kwa wasio Wakristo, hasa wamonaki wa kiume.

Maarufu sana ni mchango wao upande wa elimu, hasa katika kuokoa maandishi ya zamani na kuyanakili ili kurithisha utajiri wa ustaarabu wa Kigiriki na wa Kirumi pamoja na mapokeo ya Kikristo.

Wabenedikto walistawi katika Karne za Kati, inavyoonyesha sensa ya monasteri 14,000 zilizohesabiwa kabla ya Mtaguso wa Konstanz (1415), ambazo baadhi yake zilifikia kuwa na wamonaki zaidi ya 900.

Uanzishaji wa mashirika mapya, kama yale ya Wafransisko na Wadominiko, ulipunguza umuhimu wao, bila ya kuwamaliza.

Wabenedikto walilipatia Kanisa Katoliki Mapapa wafuatao:

Muundo wa shirika

[hariri | hariri chanzo]

Wabenedikto, wakiongozwa na abati kwa wanaume au na abesi kwa wanawake, wanaishi katika monasteri ambazo zinajitegemea kiutawala na kuunda mashirikisho 20 ya kiume.

Mnamo tarehe 31 Januari 2005 monasteri za kiume zilikuwa 349 na wamonaki 7.876, ambao kati yao 4.350 ni makasisi pia.

Wamonaki Wabenedikto wa kike mwishoni mwa mwaka huo walikuwa 4.661 katika monasteri 242, mbali na wale wa marekebisho mbalimbali, na masista wa mashirika ya Kibenedikto.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wabenedikto kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.