Jiografia ya Tanzania
Jiografia ya Tanzania inahusu nchi hiyo ambayo ina historia yake kuu ni uhuru na muungano. Kabla ya kuitwa Tanzania nchi upande wa bara iliitwa Tanganyika na ilipata uhuru tarehe 9 Desemba 1961. Baada ya uhuru wa funguvisiwa la Zanzibar, ilijihusisha katika muungano wa nchi mbili ambazo ni Tanganyika na Zanzibar zilizoungana mnamo 26 Aprili 1964 kuunda TanZanIa.
Nchi
[hariri | hariri chanzo]Tanzania ni nchi iliyomo mashariki mwa Afrika. Nchi hiyo inazungukwa na bahari upande wa mashariki, Kenya na Uganda upande wa kaskazini, Malawi upande wa kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi.
Eneo
[hariri | hariri chanzo]Tanzania ina eneo la takriban km2 947.303.
Nchi iko katika eneo la Maziwa makubwa ya Afrika, hivyo maziwa yanafunika km2 61,500, yaani 6% za eneo lote la nchi.
Pia ina mito mingi ambayo inaelekeza maji yake katika Bahari ya Hindi mashariki mwa nchi, lakini mingine inachangia Mto Zambezi kupitia Ziwa Nyasa, michache Bahari ya Kati kupitia Ziwa Victoria na mto Naili, mingine tena Bahari Atlantiki kupitia Ziwa Tanganyika na mingine inaishia katika mabonde kama ya Ziwa Rukwa.
Karibu thuluthi moja ya nchi inalindwa kwa namna moja au nyingine: kuna Hifadhi za Taifa 16, mbali ya Hifadhi Teule, Hifadhi za Mawindo, Mapori ya Akiba n.k.
Milima
[hariri | hariri chanzo]Tanzania ni mojawapo ya nchi zenye vivutio mbalimbali vya watalii kutoka maeneo mengi duniani. Vivutio hivyo ni kama vile milima, mbuga za wanyama, kumbukumbu za maisha ya watu wa kale n.k. Tanzania imebahatika kuwa na kivutio kikubwa Duniani ambacho ni Mlima Kilimanjaro, mmojawapo kati ya milima mikubwa na mirefu duniani. Mlima Kilimanjaro una urefu wa zaidi ya futi 5300 kutokea ardhini. Mlima huo unapatikana katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mbali na mlima huo wa Kilimanjaro, Tanzania inayo milima mingine kama vile Milima ya Uluguru, Milima ya Udzungwa, Mlima Oldonyo Lengai n.k.
Tabianchi
[hariri | hariri chanzo]Tabia ya nchi ya Tanzania hubadilika kwa nyakati tofautitofauti katika mwaka.
- Tanzania hupata majira ya joto katika miezi ya Desemba, Januari na Februari. Hata hivyo kiasi cha joto ni cha juu katika ukanda wa Pwani kuliko katika sehemu za nyanda za juu na milimani. Katika miezi hii jua la utosini huwa kwenye kizio cha kusini, hivyo Tanzania hupata joto zaidi.
- Katika miezi ya Juni, Julai na Agosti, kuna hali ya baridi kwa sababu wakati huu jua la utosini huwa katika kizio cha kaskazini.
- Mvua za vuli hunyesha katika miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba na mvua za masika hunyesha katika miezi ya Machi, Aprili na Mei ingawa zipo tofauti ndogo kati ya sehemu mbalimbali.
Hivyo kiasi cha mvua na halijoto husababisha tofauti za aina ya uoto wa asili, udongo na aina ya mazao yanayolimwa.
Watu
[hariri | hariri chanzo]Tanzania ina idadi kubwa sana ya watu waishio nchini, kutokana na makabila mbalimbali yaliyomo nchini, yakiwemo ya Wasukuma, Wanyamwezi, Wahaya, Waha, Wagogo, Wanyakyusa, Wahehe, Wachaga, Waluguru, Wazaramo na mengineyo.
Watu waishio nchini ni wa dini tofauti wakiwemo Waislamu (31.4%) na Wakristo (35.5%) kadiri ya sensa ya miaka ya 1960.
Marais
[hariri | hariri chanzo]Mpaka sasa muungano umekuwa na marais wanaume watano: Julius Kambarage Nyerere, Benjamin William Mkapa, Ali Hassan Mwinyi, Jakaya Mrisho Kikwete, John Pombe Magufuli, wa sita akiwa Samia Suluhu Hassan, mwanamke.
Mji mkuu
[hariri | hariri chanzo]Mji mkuu wa Tanzania ni jiji la Dodoma.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Maziwa ya Tanzania
- Mito ya Tanzania
- Orodha ya milima ya Tanzania
- Mbuga za Taifa la Tanzania
- Tabia ya nchi Tanzania
Makala hii kuhusu maeneo ya Tanzania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Jiografia ya Tanzania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno. |