Richard wa Chichester
Richard wa Chichester (1197 - Dover, 3 Aprili 1253) alikuwa askofu wa Uingereza ambaye alipigania adhimisho la ekaristi lifanyike kwa heshima, sakramenti zitolewe bure kwa waamini na makasisi washike vema useja kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.
Papa Urban IV alimtangaza kuwa mtakatifu tarehe 22 Januari 1262.
Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifo chake[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Kijana
[hariri | hariri chanzo]Ujanani alitakiwa kufanya kazi nzito ili kutegemeza familia yake. Baadaye aliweza kwenda masomoni kwenye chuo kikuu cha Oxford, chini ya Edmund Rich na Grosseteste, halafu Paris (Ufaransa) na Bologna (Italia).
Katibu mkuu wa jimbo
[hariri | hariri chanzo]Akiwa na umri wa miaka 38 akarudi Oxford, alipochaguliwa mara awe gombera wa chuo kikuu, lakini mwaka 1237 mwalimu wake wa zamani Rich, kisha kuchaguliwa Askofu mkuu wa Canterbury, alimtaka awe katibu mkuu wa jimbo lake; katika kazi hiyo alijitokeza katika jitihada za kurekebisha mwenendo wa mapadri na kupinga uvamizi wa serikali katika mamlaka ya Kanisa.
Padri
[hariri | hariri chanzo]Aliposhuhudia kifo cha askofu wake huko Soissy, Ufaransa, mwaka 1240, na kuachiwa kikombe cha Misa kama urithi, aliamua kuingia upadri akaenda kusomea teolojia miaka miwili kwa Wadominiko wa Orléans.
Baada ya kupadirishwa mwaka 1242 akiwa na miaka 45, akarudi Uingereza na kufanya kazi ya paroko Charing na Deal (mkoa wa Kent), lakini akarejeshwa mapema katika ukatibu mkuu.
Askofu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 1244 alichaguliwa na maaskofu kuongoza jimbo la Chichester, lakini mfalme Henry II alimtaka Richard Passelewe, hivyo akazuia mali na mapato ya jimbo.
Papa Inosenti IV alipoombwa usuluhisho alimtibithisha na kumweka wakfu mwaka 1245 huko Lyons.
Askofu mpya aliporudi Chichester, alilazimika kuishi kifukara katika nyumba ya paroko wa Tarring (Sussex), akifanya kazi za mikono na kutembelea jimbo lote kwa miguu. Miaka miwili baadaye mfalme Henry III alilazimishwa na Papa kulirudishia jimbo mali zote.
Matendo ya upendo
[hariri | hariri chanzo]Richard alikuwa mkarimu sana kwa fukara na mpole kwa wakosefu. Alitunga sheria za jimbo, ambazo zinadumu hadi leo, kuhusu masuala mbalimbali.
Kifo
[hariri | hariri chanzo]Akiwa Dover ili kumjengea kanisa hayati mwalimu wake Edmund Rich, aliugua sana akafa tarehe 3 Aprili 1253.
Sala yake
[hariri | hariri chanzo]Asante kwako, Bwana wangu Yesu Kristo, kwa fadhili zote ulizonistahilia.
Kwa mateso na matusi yote uliyoyavumilia kwa ajili yangu.
Mkombozi, rafiki na kaka mwenye huruma nyingi, naomba niweze kukufahamu wazi zaidi, kukupenda kwa hisani zaidi, kukufuata kwa karibu zaidi, siku kwa siku.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Atkinson, Pete. (2007). Chichester Cathedral. Norwich: Jarold Publishing. ISBN 978-0-7117-4478-3.
{{cite book}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - Diana E. Greenway (1996). "Bishops". Fasti Ecclesiae Anglicanae 1066-1300: volume 5: Chichester. Institute of Historical Research. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-08. Iliwekwa mnamo 21 Oktoba 2007.
- Bullock-Webster, G.R. (1913). The Churchman's Prayer Manual. London: Published by Author.
- Butler, Alban. Lives of the Saints. Tan Books and Publishers: Rockford, 1955
- Farmer, David Hugh (2003). "The Oxford Dictionary of Saints". Oxford University Press. Oxford Reference Online. Oxford University Press. West Sussex County Library Service. Iliwekwa mnamo 28 Januari 2011. -subscription required.
- Foster, Paul, mhr. (2009). Richard of Chichester (1197 - 1253). Chichester: University of Chichester. ISBN 978-0-948765-42-1.
- Fryde, E. B. (1996). Handbook of British Chronology (tol. la Third Edition, revised). Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 0-521-56350-X.
{{cite book}}
: Unknown parameter|coauthors=
ignored (|author=
suggested) (help) - Compiled By The Community of the Resurrection Mirfield (1922). Mirfield Mission Hymn Book. Mirfield, Yorkshire: Community of the Resurrection.
- Headlam, Cecil (1898). Prayers of Saints :Being A Manual of Devotions Compiled from the Supplications of the Holy Saints and Blessed Martyrs and Famous Men. London: F.E. Robinson.
- Hobbs, Mary, mhr. (1994). Chichester Cathedral. An Historic Survey. Chichester: Phillimore.
- "St Georges News in St George's Parish Magazine". Waterlooville, Hampshire: St Georges Church. Machi 2004. Iliwekwa mnamo 21 Oktoba 2007.
- Lawrence, C. H. (2004; online edn, Jan 2008). "'Wyche, Richard of St Richard of Chichester (d. 1253)'". Oxford Dictionary of National Biography, Oxford University Press. Iliwekwa mnamo 13 Aprili 2011.
{{cite web}}
: Check date values in:|year=
(help) - Lower, Mark Anthony (1865). The Worthies of Sussex. Lewes, Sussex: Sussex Advertiser.
- Schwartz, Simon (1971). "Godspell: Vocal Selections". Wisconsin: Hal Leonard. ISBN 978-0-88188-446-3.
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help) - Stephens, W.R.W. (1876). Memorials of the South Saxon See and Cathedral Church of Chichester. London: Bentley.
- Stephens, W.R.W. (1881). The South Saxon Diocese, Selsey - Chichester. London: SPCK.
- Roberts, Holly Harlayne (2004-09-01). Vegetarian Christian Saints: Mystics, Ascetics & Monks. New York: Anjeli Press. ISBN 978-0-9754844-0-1. Iliwekwa mnamo 2010-12-09.
- Ralph Vaughan Williams, Percy Dearmer, Martin Shaw, mhr. (1931 repr. 1963). Songs of Praise. Enlarged Edition (Full music version). Oxford: OUP. ISBN 0-19-231207-3.
{{cite book}}
: Check date values in:|year=
(help)CS1 maint: multiple names: editors list (link) - West Sussex County Council A Day To Show You're Proud Of Sussex accessed on 25 Agosti 2007
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Biography of St Richard of Chichester from Catholic Online
- St. Richard de Wyche from Catholic Encyclopedia
- St. Richard, Bishop and Confessor from The Lives of the Saints by Alban Butler
- St Richard's RC Parish, Chichester Archived 23 Januari 2022 at the Wayback Machine.
- The Parish Church of St Richard, Aldwick Archived 24 Machi 2012 at the Wayback Machine. in memory of St Richard, Bishop of Chichester 1244-1253
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |