[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Papai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Papai.

Papai ni tunda la mpapai ("Carica papaya"), mti wa familia Caricaceae. Una asili ya Amerika ya Kusini na ya Kati na unakuzwa huko Meksiko, karne kadhaa kabla ya kuibuka kwa tamaduni mpya za huko Amerika.

Ni mti mrefu wenye shina la urefu wa mita 5 mpaka 10, wenye majani yaliyojipanga yaliyojizungusha na kujishikiza juu kwenye shina la mti, shina kwa upande wa chini huwa na makovu mengi kuonesha sehemu ambayo majani yalikuwa. Majani ya mpapai ni makubwa sm 50 – 70 kwa upana, maua yake ni madogo na hutokea sehemu yalipochomoza majani, hutengeneza tunda papai lenye urefu wa sm 15- 45, na upana wa sm 10 – 30.

Tunda huiva pale linapokuwa laini (kama vile parachichi au zaidi) na ngozi yake inapokuwa na ngozi yake inapokaribia rangi ya chungwa ladha ya chungwa hukamilana na ile kati ya nanasi na peasi, ingawa huwa ya utulivu bila ya uchungu wowote.

Wingi na matumizi ya papai

[hariri | hariri chanzo]

Kutoka asili yake ya Meksiko, Puerto Rico, Amerika ya Kati na kusini mwa Asia.

Papai lililoiva huliwa bila ya maganda wala mbegu zake; papai bichi huliwa baada ya kuchemshwa na kupimwa pamoja na saladi ya michemsho mingine.

Papai bichi na mti wake huwa na utomvu wenye kemikali inayoitwa papaini ambayo hutumika kulainisha nyama kwa kuvunjavunja protini iliyo ndani yake. Uwezo wake huu wa kulainisha nyama ngumu umetumiwa na watu wa kale tangu enzi za zamani.

Tafiti mbalimbali zimeonesha kwamba mbegu za papai ni muhimu kwa afya ya binadamu kuliko papai lenyewe; zinaweza kutibu matatizo ya ini, figo, malaria, baadhi ya minyoo na hupunguza unene uliopitiliza.

Wanawake huko Uhindi, Pakistani na Sri Lanka walitumia sana papai kama njia ya kuzuia mimba na hata kutoa mimba wanawake waliokuwa utumwani ai pia walionekana sana wakitumia sana papai ili kuzuia wasishike mimba na kuwazaa watoto wao utumwani imegundulika hata mbegu za papai nazo huweza kusababisha kuondoa uwezo wa kuzaa kwa wanaume.

Shina na matawi ya mipapai pia yanatumika kutengenezea kamba. Mbegu zaidi za mipapai huweza kuliwa na zina ladha kali sana. Husagwa na wakati mwingine kutumiwa kama mbadala wa pilipili. Sehemu fulani za Asia, majani machanga ya mpapai huchemshwa kwa mvuke na kuliwa kama spinachi. Sehemu fulani duniani majani ya mpapai hunyweshwa na chai kama dawa ya kutibu malaria, japo hakuna ushahidi wa kutosha juu ya matibabu haya.

Hatari ya matumizi ya papai na mazao yake

[hariri | hariri chanzo]

Tunda la papai, mbegu na utomvu wake, pia majani yake yana kiwango kikubwa cha carpaine, kemikali inayoondoa minyoo kwenye mwili lakini matumizi ya kiasi kikubwa huweza kuwa hatari.

Inafahamika kuwa mapapai mabichi yanaweza kusababisha kutoka kwa mimba kutokana na kiwango kikubwa cha kemikali ya Latex ambayo husababisha kuta za uterasi kusinyaa japo haijathibitishwa bado.

Kula sana mapapai kama ilivyo kwa karoti, huweza kusababisha ugonjwa wa karotinemia ambapo nyayo na viganja huwa vya rangi ya njano japo hakuna madhara yoyote.