Sekta ya viwanda
Sekta ya viwanda ni sehemu muhimu ya uchumi wa kisasa ambako bidhaa zinatengenezwa kwa wingi kwa kutumia mashine na michakato maalumu.
Viwanda huhesabiwa kati ya shughuli za sekta ya upili ya uhumi kwa jumla ambako malighafi zinabadilishwa kuwa bidhaa, kwa mfano chuma kuwa feleji na vifaa mbalimbali au pamba kuwa kitambaa na nguo. Viwanda si sehemu ya pekee ya sekta ya upili kwa mfano kuna mafundi wanaotengeneza pia bidhaa kutokana na malighafi kwa mfano wahunzi au wafumaji. Viwanda hutumia zaidi mashine, hupanga michakato yake kikamilifu na kutoa bidhaa zisizosanifishwa kwa wingi kabisa.
Aina za viwanda
[hariri | hariri chanzo]Aina za viwanda hutofautishwa kutokana na malighafi zinazotumia hasa kama vile
- viwanda vya kutengeneza feleji kutokana na malighafi asilia chuma na makaa mawe
- viwanda vya kutengeneza bidhaa za metali kutokana na feleji kama vile mashine, magari, meli, vifaa vya umeme
- viwanda vya kemia vinavyotumia malighafi kama mafuta ya petroli na minerali pamoja na madawa mbalimbali vikitoa kwa mfano mbolea, saruji, karatasi, plastiki, petroli au dawa za tiba.
- viwanda vya kutolea bidhaa za matumizi ya kila siku kama vile vyakula, nguo, fenicha, magazeti, vitabu au mahitaji ya ofisi.
Mfumo wa viwanda
[hariri | hariri chanzo]Viwanda kwa maana ya kisasa vimejitokeza tangu kupatikana kwa mashine hasa tangu karne ya 19. Kupatikana kwa mashine ya mvuke kulirahisisha gharama za kutengeneza kwa vitu na kusababisha mapinduzi ya viwanda yaliyoanza nchini Uingereza yakisambaa haraka Ulaya na Marekani.
Sekta ya viwanda ilipanua sana katika karne ya 19 hadi katikati ya karne ya 20; katika nchi zilizoendelea karibu nusu ya wafanyakazi wote walikuwa katika sekta hii. Ila tu tangu nusu ya pili ya karne ya 20 sekta ya tatu na ya nne yaani biashara na huduma zilianza kuwa na wafanyakazi wengi zaidi. Hii ni tokeo la kufanyikiwa kwa viwanda vinavyoendelea kutoa bidhaa nyingi haraka kwa kuhitaji wafanyakazi wachache kulko zamani kwa sababu uwezo wa mashine imeongezeka.
Kwa upande wa Tanzania na nchi nyingine duniani kuna viwanda vichache zaidi; hiyo inasababisha watu wengi kukosa ajira.