Majadiliano ya mtumiaji:Hamisj
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Kipala (majadiliano) 20:12, 11 Julai 2019 (UTC)
Kurasa za Vyuo
[hariri chanzo]Habari umeanzisha leo makala ya Chuo Kikuu cha Arusha. Lakini uliiacha katika hali isiyo na maana na haitamsaidia mtu yeyote. Nakupongeza kwa nia yako kutunga makala za vyuo vya Tanzania ambayo ni kitu kizuri, asante! Ila tu usilete makala zisizo na habari yoyote na hivyo kukosa maana. Ungeweza kutafsiri (hata ukifupisha) makala ya Kiingereza en:University_of_Arusha. Makala angalau iwe na mambo ya kimsingi ni chuo cha nani, kinafundisha masomo gani, kuonyesha tovuti yake na rejeo kwa ukurasa wa TCU linalothibitisha linatambuliwa hapa TZ - ii tusipate tena makala kama ile kuhusu Baptist University. Tafadhali usahihishe haraka ili tusipaswe kuweka onyo la kufuta. Kipala (majadiliano) 09:32, 22 Novemba 2019 (UTC)
Habari, Bado niko naandika, ila kwa kua niko ofisini nilipata kufanya kazi nyingine kwa hiyo nikawa nime-save pale ilipofikia ili nisianze upya nikirudi katika kurasa. Asante kwa ujumbe
- Basi jaribu njia hii:unda ukurasa wa muda kama unashindwa kumaliza. Fungua "https://sw.wikipedia.org/wiki/Mtumiaji:Hamisj" halafu katika mstari wa anwani ongeza "/test" au kwa mfano huu "/Chuo Kikuu cha Arusha". hapa unaanzisha ukurasa mpya ndani ya himaya yako. Baada kumaliza utainakili na kupeleka mahali penyewe. Ninatumia njia hii mara kwa mara. Kipala (majadiliano) 13:26, 22 Novemba 2019 (UTC)
Asante, nilikua sijui hii njia. Umekua mwalimu mzuri na kosa langu limekua funzo, nitakua nikitumia njia hiyo sasa. Maana mara nyingi hua ninasumbuka namna ya kuandaa draft kabla ya kuifanya makala.