Imani ya Athanasio
Imani ya Athanasio (pia: Quicumque vult, kutokana na maneno ya kwanza ya Kilatini Quicumque vult salvus esse) ni mojawapo ya maungamo ya imani makuu ya imani ya Kikristo yanayokubaliwa katika makanisa ya magharibi, pamoja na Imani ya Mitume na Imani ya Nikea. [1] Inakazia mafundisho kuhusu Utatu wa Mungu na hali mbili za Yesu Kristo.
Historia ya matini
Katika mapokeo ya kanisa la magharibi, Athanasio wa Aleksandria (karne ya 4 BK) hutajwa kama mwandishi wa maungamo hayo. Maazimio ya Mtaguso wa Autun (mnamo 670 nchini Ufaransa) yalitaja mara ya kwanza "Imani ya Mtakatifu Athanasio" [2] na hapo inawezekana kwamba yalilenga matini ya "Quicumque".
Ila tangu karne ya 17 inajulikana kwamba matini hayo hayakutungwa na Athanasio[3]. Ni dhahiri kwamba ilitungwa kwa lugha ya Kilatini ilhali Athanasio hakutumia Kilatini akaandika kwa lugha ya Kigiriki. Vilevile matini yake yanakosa istilahi zilizokuwa muhimu kwa Athanasio kama vile homoousion, lakini inataja "Filioque" ambayo ni kawaida ya kanisa la magharibi ikikataliwa katika Ukristo wa Mashariki.[4] Pia ungamo hilo halijulikani katika Makanisa ya Mashariki, ingawa jina la Athanasius linaheshimiwa sana huko.
Inaonekana kwamba kwamba matini ya maungamo yaliunganishwa kwa kutumia nukuu kutoka kwa Mababu wa Kanisa la Kilatini (hasa mapokeo ya Augustino) kama vile Ambrosio wa Milan, Vincent wa Lérins, Fulgensyo wa Ruspe na hatimaye Caesarius wa Arles .
Muundo
Ungamo lina aya arobaini zilizogawanywa katika sehemu kuu mbili tofauti:
- Sehemu ya kwanza inatoa fundisho la Mungu kama Utatu. Maneno yake huonyesha ushawishi wa theolojia ya Agostino wa Hippo na kujitofautisha na Umodali na Uario .
- Sehemu ya pili inasisitiza imani katika Umwilisho huku ikijitenga na mafundisho ya Sabelio, Apolinari wa Laodikea, Ario, na Wamonofisiti.
Matini kamili
Kilatini (kufuatana na Liber Usualis) | Kiswahili (kufuatana na Tumwabudu Mungu Wetu)[5] |
---|---|
Quicumque vult salvus esse, ante omnia opus est, ut teneat catholicam fidem: |
Kila atakaye kuokoka: Zaidi ya yote imemlazimu kuishika Imani Katholiko |
Quam nisi quisque integram inviolatamque servaverit, absque dubio in aeternum peribit. |
Ambayo, asipoihifadhi kamili na bila kuiharibu: bila shaka atapotea milele. |
Fides autem catholica haec est: ut unum Deum in Trinitate, et Trinitatem in unitate veneremur: |
Na Imani Katholiko ndiyo. hii: Tumwabudu Mungu mmoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja. |
Neque confundentes personas, neque substantiam separantes. |
Tusizichanganye nafsi: Wala kuugawanya Uungu. |
Alia est enim persona Patris, alia Filii, alia Spiritus Sancti. |
Kwa maana Nafsi ya Baba mbali, Nafsi:ya Mwana mbali: Na Nafsi ya Roho Mtakatifu mbali. |
Sed Patris, et Filii, et Spiritus Sancti una est divinitas, aequalis gloria, coeterna maiestas. |
Bali Uungu wa Baba, na wa Mwana, na wa Roho Mtakatifu ni Uungu mmoja; Utukufu wao ni sawa, Ukuu wao ni wa milele. |
Qualis Pater, talis Filius, talis Spiritus Sanctus. |
Kama alivyo Baba, ndivyo alivyo Mwana: Ndivyo alivyo Roho Mtakatifu. |
Increatus Pater, increatus Filius, increatus Spiritus Sanctus. |
Baba hakuumbwa, Mwana hakuumbwa: Roho Mtakatifu hakuumbwa. |
Immensus Pater, immensus Filius, immensus Spiritus Sanctus. |
Baba hana mpaka, Mwana hana mpaka: Roho Mtakatifu hana mpaka. |
Aeternus Pater, aeternus Filius, aeternus Spiritus Sanctus. |
Baba ni wa milele, Mwana ni wa milele; Roho Mtakatifu ni wa milele. |
Et tamen non tres aeterni, sed unus aeternus. |
Walakini hakuna watatu walio wa milele: Bali Mmoja aliye wa milele. |
Sicut non tres increati, nec tres immensi, sed unus increatus, et unus immensus. |
Kadhalika hakuna watatu wasioumbwa, wala watatu wasio na mpaka: Bali asiyeumbwa ni mmoja tu, na asiye na mpaka ni mmoja tu. |
Similiter omnipotens Pater, omnipotens Filius, omnipotens Spiritus Sanctus. |
Kadhalika Baba ni Mwenyezi, Mwana Mwenyezi: Na Roho Mtakatifu Mwenyezi. |
Et tamen non tres omnipotentes, sed unus omnipotens. |
Walakini hakuna watatu walio Wenyezi: Bali aliye Mwenyezi ni mmoja tu. |
Ita Deus Pater, Deus Filius, Deus Spiritus Sanctus. |
Vivyo hivyo Baba ni Mungu, Mwana ni Mungu: Na Roho Mtakatifu ni Mungu. |
Et tamen non tres Dii, sed unus est Deus. |
Walakini hakuna Mungu watatu: Ila aliye Mungu ni mmoja tu. |
Ita Dominus Pater, Dominus Filius, Dominus Spiritus Sanctus. |
Vivyo hivyo Baba ni Bwana, na Mwana ni Bwana: Na Roho Mtakatifu ni Bwana. |
Et tamen non tres Domini, sed unus est Dominus. |
Walakini hakuna Mabwana watatu: Bali Bwana ni mmoja tu. |
Quia sicut singillatim unamquamque personam Deum ac Dominum confiteri christiana veritate compellimur: ita tres Deos aut Dominos dicere catholica religione prohibemur. |
Kwa maana kama tunavyoshurutishwa kwa kanuni ya kweli ya Kikristo: Kukiri ya kuwa kila Nafsi ni Mungu na Bwana. Kadhalika tunagombezwa na Imani Katholiko: Tusiseme ya kuwa wako Miungu watatu au Mabwana watatu. |
Pater a nullo est factus: nec creatus, nec genitus. |
Baba hakuumbwa na aliye yote: Hakuhulukiwa wala hakuzaliwa. |
Filius a Patre solo est: non factus, nec creatus, sed genitus. |
Mwana anatoka katika Baba tu: Hakuumbwa; wala hakuhulukiwa, bali yu Mwana wa azali. |
Spiritus Sanctus a Patre et Filio: non factus, nec creatus, nec genitus, sed procedens. |
Roho Mtakatifu anatoka katika Baba na Mwana: Hakuumbwa wala hakuhulukiwa, wala hakuzaliwa; bali anatoka. |
Unus ergo Pater, non tres Patres: unus Filius, non tres Filii: unus Spiritus Sanctus, non tres Spiritus Sancti. |
Basi yupo Baba mmoja tu, si Baba watatu; yupo Mwana mmoja tu, si Wana watatu: Yupo Roho Mtakatifu mmoja hu; si Roho Watakatifu watatu. |
Et in hac Trinitate nihil prius aut posterius, nihil maius aut minus: sed totae tres personae coaeternae sibi sunt et coaequales. |
Na katika Utatu huu hapana aliye wa kwanza na aliye wa baadaye: Hapana aliye mkuu zaidi na aliye mdogo. Bali Nafsi zote tatu ni wa milele: Wa sawa wote. |
Ita ut per omnia, sicut iam supra dictum est, et unitas in Trinitate, et Trinitas in unitate veneranda sit. |
Basi, katika mambo yote kama tulivyokwisha kusema: Imetupasa kuuabudu Umoja katika Utatu, na Utatu katika Umoja. |
Qui vult ergo salvus esse, ita de Trinitate sentiat. |
Kwa hiyo yeye atakaye kuokoka: Na aone hivyo juu ya Utatu. |
Sed necessarium est ad aeternam salutem, ut Incarnationem quoque Domini nostri Iesu Christi fideliter credat. |
Na zaidi ya hayo, ili apate wokovu wa milele: Imempasa kuamini kwa moyo Kufanyika mwili kwake Bwana wetu Yesu Kristo. |
Est ergo fides recta, ut credamus et confiteamur, quia Dominus noster Iesus Christus Dei Filius, Deus et homo est. |
Na Imani kamili ndio hii; Tuamini na kukiri ya kuwa Bwana wetu Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, ni Mungu na Mwanadamu. |
Deus est ex substantia Patris ante saecula genitus: et homo est ex substantia matris in saeculo natus. |
Yu Mungu, ana Uungu wa Baba, yu Mwana kabla ya zamani zote: Ni Mwanadamu, ana utu wa mama yake, alizaliwa katika ulimwengu. |
Perfectus Deus, perfectus homo: ex anima rationali et humana carne subsistens. |
Mungu kamili na Mwanadamu: Ana roho yenye akili na mwili wa kibinadamu. |
Aequalis Patri secundum divinitatem: minor Patre secundum humanitatem. |
Yu sawa na Baba kwa kuwa ni Mungu: Yu chini ya Baba kwa kuwa ni Mwanadamu. |
Qui, licet Deus sit et homo, non duo tamen, sed unus est Christus: |
Na ijapokuwa yu Mungu tena Mwanadamu: Yeye si wawili; bali ni Kristo mmoja. |
Unus autem non conversione divinitatis in carnem, sed assumptione humanitatis in Deum: |
Yeye ni mmoja, si kana kwamba Uungu umebadilika uwe mwili: Bali kwa kuutwaa utu wa mwanadamu na kuuunga na Mungu. |
Unus omnino non confusione substantiae, sed unitate personae. |
Mmoja kabisa, si kwa kuuchanganya Uungu na utu: Bali kwa kuwa Nafsi mmoja tu. |
Nam sicut anima rationalis et caro unus est homo: ita Deus et homo unus est Christus. |
Kwa maana kama vile nafsi yenye akili pamoja na mwili huwa mwanadamu mmoja: Kadhalika Mungu na Mwanadamu pamoja ni Kristo mmoja. |
Qui passus est pro salute nostra, descendit ad inferos: tertia die resurrexit a mortuis. |
Aliyeteswa kwa wokovu wetu: Akashuka mahali pa wafu, akafufuka
siku ya tatu. |
Ascendit ad caelos, sedet ad dexteram Dei Patris omnipotentis: inde venturus est iudicare vivos et mortuos. |
Akapaa mbinguni, ameketi mkono wa kuume wa Baba, Mungu Mwenyezi: Kutoka huko atakuja kuwahukumu waliohai na waliokufa. |
Ad cuius adventum omnes homines resurgere habent cum corporibus suis: et reddituri sunt de factis propriis rationem. |
Naye atakapokuja, wanadamu wote watafufuliwa na miili yao: Nao watatoa habari za matendo yao. |
Et qui bona egerunt, ibunt in vitam aeternam: qui vero mala, in ignem aeternum. |
Nao waliotenda :mema wataingia katika Uzima wa milele: Nao waliotenda mabaya katika moto wa milele. |
Haec est fides catholica, quam nisi quisque fideliter firmiterque crediderit, salvus esse non poterit. |
Hii ndiyo Imani Katholiko: Ambayo mtu asipoisadiki kwa uuaminifu hawezi kuokoka. |
Matumizi makanisani
Wakati wa Matengenezo ya Kiprotestanti imani hiyo ilihesabiwa kama moja ya maungamo makuu matatu yaliyotumiwa makanisani. Kanisa la Kiinjili la Kilutheri limelipokea kati ya maungamo yake na pia Wareformed wanalitambua.
Kwa sasa inatumika katika liturujia ya makanisa ya Kianglikana; liko pia katika kitabu cha "Tumwabudu Mungu wetu" wa KKKT.
Lilikuwa sehemu ya liturujia ya sala ya asubuhi ya saa 12 (prim) katika Kanisa Katoliki; tangu kuondolewa kwa utaratibu huo kutoka Liturujia ya Vipindi matini ya Quicumque vult yanatumika na wachache tu.
Tanbihi
- ↑ https://web.archive.org/web/20050429143510/http://www.vatican.va/archive/DEU0035/_P1B.HTM Katechismus der Katholischen Kirche, Artikel 193
- ↑ Hubert Mordek: Kirchenrecht und Reform im Frankenreich. Die Collectio Vetus Gallica, die älteste systematische Kanonessammlung des fränkischen Gallien. Berlin 1975, S. 84ff.
- ↑ O'Carroll, Michael (1987), "Athanasian Creed", Trinitas, Collegeville: Liturgical Press, ISBN 0814655955
- ↑ Norris, Frederick (1997), "Athanasian Creed", in Ferguson, Everett (ed.), Encyclopedia of Early Christianity (2nd ed.), uk. 110, New York: Garland, ISBN 0824057457, [https://archive.org/details/encyclopediaofea0000unse/page/110/mode/2up online hapa]
- ↑ Matini iliyochapishwa katika kitabu cha Tumwabudu Mungu Wetu 2012, kilichotolewa na KKKT, ISBN 9987-652-08-5
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Imani ya Athanasio kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |