[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

I Ain't Mad at Cha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
“I Ain't Mad at Cha”
“I Ain't Mad at Cha” cover
Single ya 2Pac akishirikiana na Danny Boy
kutoka katika albamu ya All Eyez on Me
Imetolewa 15 Septemba 1996
Muundo 12" single, CD single
Imerekodiwa Oktoba 1995
Aina Rap
Urefu 4:53
Studio Death Row/Interscope
Mtunzi T. Shakur
D. Stewart
D. Arnaud
E. Jordan
Mtayarishaji Daz Dillinger
Mwenendo wa single za 2Pac
"All Bout U"
(1996)
"I Ain't Mad at Cha"
(1996)
"Life Goes On"
(1996)

I Ain't Mad at Cha ni jina la kutaja wimbo wa rapa 2Pac. Wimbo ulitolewa ukiwa kama single ya nne kutoka katika albamu yake ya All Eyez on Me. Japokuwa wimbo ulitolewa miezi saba kamili kabla ya kifo chake kutokea, lakini kutolewa kama single muda mfupi baada ya kifo chake. Wimbo aliutoa hasa kutoka moyoni mwake akiwalenga wamarafiki zake aliowajua kabla hajawa maarufu. Wimbo umemshirkisha mwimbaji muziki wa R&B na soul Danny Boy ambaye ametoa kiitikio cha wimbo. Wimbo umefanya vizuri nchini Uingereza, kwa kufikia nafasi ya 13 kwenye UK Singles Chart. Haikutolewa kama single nchini Marekani, hivyo ukaufanya wimbo usifae kwenye chati za single za Billboard (kwa kutokana na sheria za chati za wakati huo), lakini ilifikia namba 18 na 58 kwenye chati za R&B na Pop Airplay, mtiririko.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wimbo ulitayarishwa na Dat Nigga Daz (ambaye kwa sasa anakwenda kwa jina la Daz Dillinger) na kuchukua sampuli ya wimbo wa "A Dream" wa DeBarge. Wimbo ulirekodiwa siku moja na ile ambayo 2Pac alitoka jela, na ulikuwa wa pili kurekodiwa pale alipotoka na ("Ambitionz Az a Ridah" kuwa wa kwanza).[1] Wimbo ulitolewa siku mbili baada ya kifo cha 2Pac. Kwa maana hiyo, kwa kipindi ambacho single hii inatolewa, 2Pac tayari amesha-maliza kurekodi albamu yake ijayo, The Don Killuminati: The 7 Day Theory. Ilipachikwa jina na wengi kwamba ni moja kati ya nyimbo bora za kwenye albamu ya "All Eyez on Me"[2] na moja kati ya kazi bab-kubwa ya 2Pac.

Wimbo huu pia umeonekana kwenye albamu ya Vibao Vikali vya 2Pac. Wimbo mwingine kutoka kwenye CD single uliodaiwa na mashabiki kuwa maarufu. "Heartz of Men" umeonekana kwenye albamu 4 za 2Pac, ukilinganisha na 3 za I Ain't Mad at Cha. Hii ni pamoja na: All Eyez on Me, 2Pac Live, 2Pac's Greatest Hits, na toleo la remixi kwenye Nu-Mixx Klazzics. Remix ilifanywa na Rihanna kwenye We Ride kwa kuingizia elementi za wimbo wa I Ain't Mad at Cha. Kundi la R&B BLACKstreet wametumia mlio wa kinanda cha wimbo huu kwa ajili ya wimbo wao wa "Don't Leave Me" kutoka kwenye albamu yake ya Another Level. "American Dream," wimbo uliomshrikisha marehemu rapa Big L In Memory of Big L, Vol.2 ime-sampo kibao cha I Ain't Mad at Cha track.

Mashairi na Ujumbe

[hariri | hariri chanzo]

Wimbo huu umekuwa kama ukumbusho namna gani wakati ulivyobadilika wakati alipokuwa mtoto na kuja katika umaarufu. Anazungumzia jinsi anavyopoteza mawasiliano na watu na watu wangapi wamem-badilikia baada ya kupata mafanikio yake. Bado anasisitiza kuboresha ujamaa wake na kusema kwamba hana "lolote bali upendo" kwa marafiki zake wa awali, na kiitikio kinachorudia mstari wa "I ain't mad at cha".

Mstari wa kwanza anazungumzia jinsi alivyopoteza mawasiliano na rafiki yake, ambaye amebadili dini na kuwa Mwislamu (inawezekana ana-maanisha kwa Napoleon, ambaye alikuwa mmoja kati ya wanachama wa kundi la Outlawz na kuamua kujiunga na imani ya Kiislamu), na utofauti wa mtindo wa kimaisha walioamua kuishi:

"Now the whole shit's changed, and we don't even kick it

Got a big money scheme, and you ain't even with it
Hmm, knew in my heart you was the same motherfucker that
Go toe to toe when it's time for roll you got a brother's back
And I can't even lie, cause ain't laughin at cha

You tryin hard to maintain, but go head cause I ain't mad at cha"

Mstari wa pili anazungumzia kuhusu 2Pac ku-hukumiwa jela. Amemtaja mwanamke wake wa zamani na amejaribu kumfariji mama yake.

"And even though we separated, you said that you'd wait

Don't give nobody no coochie while I be locked up state
I kiss my Mama goodbye, and wipe the tears from her lonely eyes
Said I'll return but I gotta fight the fate's arrived
Don't shed a tear, cause Mama I ain't happy here

I'm through trial, no more smiles, for a couple years"

Katika mstari wa tatu, 2Pac anarap kuhusu maisha yake jinsi yalivyobadilika kuanzia maisha ya ghetto hadi kuwa mtu mashuhuri. Anazungumzia mahusino yake na majirani na jumuia yake ya zamani jinsi wanavyomfikiria sivyo kwa sasa.

"So many questions, and they ask me if I'm still down

I moved up out of the ghetto, so I ain't real now?
They got so much to say, but I'm just laughin at cha

You niggaz just don't know, but I ain't mad at cha"

Muziki wa Video

[hariri | hariri chanzo]
music video screenshots

Kama jinsi ilivyo nyimbo nyingi za rap, single ina-mashairi mengi sana yasiyopendeza kwa jamii na ulikuwa haoneshwi sana kwenye TV. Licha ya maneno yale kutolewa, mara mistari hii huchukuliwa kwa maana nyingine. Kwa mfano:

Mashairi halisi yanasema: And I can see us after school, we'd bomb / on the first motherfucker with the wrong shit on

Mashari badala yake: And I can see us after school, we'd bomb / on the first player haters with the wrong set on.

Muziki wa video unaaza na 2Pac na rafiki yake (imechezwa na Bokeem Woodbine) wanatoka kwenye sherehe nyakati za usiku. Wakati wanasubiri kuianza safari ya kwenda nyumbani, mtu mmoja aliyejifunika na kofia anafika na kutoa pistol na kupiga kuelekea upande wao. Wakati 2Pac anajaribu kuwasukumia nje, akapigwa angalau na risasi moja. Wakiwa ndani ya ambulance, nafsi yake imetoka na kupelekea kufariki. Akiwa kama malaika aliyerudi Duniani na kumtazama rafiki jinsi anavyoangaika kuimaliza siku zilizofuata kuwa mbali na rafiki yake. Wakati hili linaendela 2Pac anaonekana akirap kwa rafiki yake, (ambaye hawezi kumwona wala kumsikia) na akiwa kwenye sherehe nzuri huko Mbinguni. Wanaonekana kama wanamuziki wengi waliokufa - wakipiga biti kwenye sherehe hiyo, wanamuziki hao ni pamoja na Jimi Hendrix, Bob Marley, Nat King Cole, Miles Davis, Marvin Gaye, na Louis Armstrong. Danny Boy pia amewakilisha Mbinguni akiwa kama malaika.

Orodha ya nyimbo

[hariri | hariri chanzo]

CD single

[hariri | hariri chanzo]

DRWCD5/854 843-2

  1. "I Ain't Mad at Cha" - Edit
  2. "I Ain't Mad at Cha" - LP Version
  3. "Skandalouz"
  4. "Heartz of Men"

12" maxi single

[hariri | hariri chanzo]

12 DRW5/854 843-1

  1. "I Ain't Mad at Cha" - Edit
  2. "I Ain't Mad at Cha" - LP Version
  3. "Skandalouz"
  4. "Heartz of Men"

Cassette single

[hariri | hariri chanzo]

DRWMC5/854 842-4

  1. "I Ain't Mad At Cha" (Edit)
  2. "Skandalouz"

Tanbihi na marejeo

[hariri | hariri chanzo]
  1. http://www.hitemup.com/newsarchives/news-archive-9-2004.html Archived 13 Oktoba 2007 at the Wayback Machine. URL accessed on 27 Septemba 2006
  2. "All Eyez on Me review".