Historia ya Turkmenistan
Historia ya Turkmenistan inahusu historia ya eneo ambalo leo linaunda jamhuri ya Turkmenistan.
Turkmenistan ilitwaliwa na Urusi tangu mwisho wa karne ya 19 ikaingia hivyo katika Umoja wa Kisovyeti baada ya mwaka 1917 na kuwa jamhuri ndani yake kwa jina la Jamhuri ya Kisovyeti ya Kijamii ya Kiturkmeni hadi mwaka 1991.
Wakati wa kusambaratika kwa Umoja wa Kisovyeti, kiongozi wa chama cha kikomunisti Saparmirat Niyasov akaendelea kushika uongozi akitawala kama rais hadi kifo chake mwaka 2006.
Niyasov alibadilisha utawala wa chama cha kikomunisti kuwa udikteta wake mwenyewe. Akaanza kutumia jina la "Turkmenbashi" (Baba wa Waturkmeni wote) na sanamu zake zikasimamishwa kote nchiniː mara nyingi zilikuwa sanamu za dhahabu hata kama wananchi walikuwa na maisha magumu.
Mapato kutoka gesi na mafuta ya petroli yalimwezesha kuendesha uchumi wa nchi kwa hiari yake bila mabadiliko makubwa jinsi ilivyokuwa kawaida wakati wa anguko la ukomunisti kwingineko.
Zaidi ya nusu ya wananchi walikuwa hawana ajira na kuishi maisha ya umaskini, lakini wanapewa chumvi, umeme na maji bure. Mkate na petroli zinauzwa kwa bei ya chini sana, lakini kuna uhaba wa mara kwa mara.
Baada ya kifo cha Niyasov kamati ya viongozi ilimteua makamu wa waziri mkuu Gurbanguly Berdimuhammedov kuwa rais mpya ingawa kadiri ya katiba mwenyekiti wa bunge alitakiwa kuchukua nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa bunge alishtakiwa mahakamani juu ya makosa fulani na Berdimuhammedov alithibitishwa katika uchaguzi wa tarehe 11 Februari 2007 kwa 89% za kura. Watazamaji walidai kura ilikuwa ya uwongo.
Mwaka 2013 kwa mara ya kwanza ulifanyika uchaguzi wa vyama vingi.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Historia ya Turkmenistan kama enzi zake au matokeo yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |