[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Hispaniola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hispaniola

Hispaniola (kutoka matamshi ya Kilatini ya jina la Kihispania "La Española" = "cha Kihispania") ni kisiwa kikubwa cha pili katika Karibi kikiwa na eneo la km² 74,700.

Iko kati ya Kuba upande wa magharibi na Puerto Rico upande wa mashariki.

Hispaniola huhesabiwa kati ya visiwa vya Antili Kubwa. Ni kile chenye watu wengi zaidi katika Amerika, na cha kumi duniani.

Mashariki mwa kisiwa yalitawaliwa na Hispania kama koloni la Santo Domingo, ilhali Wafaransa walianzisha koloni lao upande wa magharibi wa kisiwa kwa jina la Saint Domingue.

Hivyo leo kisiwani kuna nchi huru mbili: Haiti upande wa magharibi na Jamhuri ya Dominikana upande wa mashariki.

Nchi Wakazi
(2005-07-01 kadirio)
Eneo
(km²)
Msongamano
wa watu(kwa km²)
Haiti 9,996,731 27,750 350.27
Jamhuri ya Dominikana 9,445,281 48,730 197
Kisiwa chote 19,442,012 76,480 254.21

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Hispaniola kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.