[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Helen Keller

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Helen Keller
Helen Keller
Helen Keller
Jina la kuzaliwa Helen Keller
Alizaliwa 27 Juni 1880
Alikufa 1 Juni 1968
Nchi Marekani
Kazi yake Mwandishi
Mwanaharakati

Helen Adams Keller (27 Juni 18801 Juni 1968) alikuwa mwandishi na mwanaharakati wa haki za binadamu kutoka nchini Marekani. Wakati alivyofikisha umri wa miezi kumi na tisa akawa anaumwa na kukapelekea kuwa na matatizo ya kutosikia na kutoona. Aliendelea kuwa mtu wa kwanza kiziwi na kipofu aliyefaulu kuchukua digrii ya chuoni.

Maisha yake

[hariri | hariri chanzo]

Helen alipokuwa na umri wa miaka saba, familia yake ikaamua kumtafutia mwalimu ambaye atakuwa akimfundisha. Wakamwomba Michael Anegnos, ambaye alikuwa mkurugenzi wa Taasisi ya Kutunza Viziwi na Vipofu. Wakamwomba awatafutie mwalimu atakayekuwa anamfundisha binti yao.

Akawakubalia na kuwaeleza kwamba anamfahamu mwanadada mmoja ambaye anajulikana kwa jina la Anne Sullivan, yeye atafaa kuwa mwalimu wa binti yenu. Baada ya hapo Anne akasafiri kuelekea mjini Alabama kwenda kuishi na familia ya akina Helen kwa lengo la kumfunza. Anne alianza rasmi kuishi na familia ya Keller kunako mwezi Machi ya mwaka wa 1887.

Anne alimsaidia Helen namna ya kuwasiliana na watu wengine. Alimfundisha majina ya vitu kwa kuandika katika kiganja cha Helen. Mnamo mwaka 1890, familia ya Helen walimpeleka mtoto wao katika Taasisi ya Viziwi na Watu Wasioona ili aweze kujifunza namna ya kuzungumza na kuweza kupata mawasiliano.

Alivyofikisha umri wa miaka kumi na tisa, Helen alielekea katika chuo kimoja kiitwacho Radcliffe cha mjini Massachusetts. Na akahitimu masomo yake katika Radcliffe kunako mwaka wa 1904. Alikuwa mtu wa kwanza katika watu vipofu na viziwi kupata digrii moja ya sanii.

Mnamo mwaka wa 1903, Helen alitunga kitabu kinachohusu maisha yake. Kitabu kilikwenda kwa jina la "The Story of My Life" (Hadithi ya Maisha Yangu). Kisha akaandika vitabu vingine kumi na viwili. Baadhi ya vitabu vyake vikaja kuigizwa katika filamu, kama vile kitabu cha "The Miracle Worker", filamu ilichezwa mnamo mwaka 1962.

Wakati wa uhai wake Helen, alijaribu kusaidia watu masikini na baadhi ya watu walio viziwi na vipofu. Helen alitembelea takriban nchi 39 akiwa pamoja na Anne kwa lengo la kuelezea habari za maisha yake na uzoefu pia. Helen pia alitunga kitabu kinachohusu maisha ya Anne Sullivan, kitabu kilikwenda kwa jina la "Teacher". Helen Keller alifariki dunia mnamo tarehe moja ya mwezi wa sita katika mwaka wa 1968, mjini Connecticut, Marekani.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Keller katika IMDB

[hariri | hariri chanzo]

Habari kuhusu siasa za Keller

[hariri | hariri chanzo]