[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Barraba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Barraba
Barraba is located in Australia
Barraba
Barraba
Majiranukta: 30°22′42″S 150°36′38″E / 30.37833°S 150.61056°E / -30.37833; 150.61056
Nchi Australia
Majimbo New South Wales
Manispaa Tamworth Regional Council
Idadi ya wakazi (2016)
 - Wakazi kwa ujumla 1,410[1]
Tovuti:  (Kiingereza) barraba.com.au

Barraba ni kijiji katika mkoa wa New England huko New South Wales, Australia. Kijiji kilikuwa kijiji kikuu cha manispaa ya Barraba Shire lakini kijiji na manispaa yake ziliungamanishwa katika manispaa ya Tamworth Regional Council (kwa Kiswahili: Halmashauri ya Mkoa wa Tamworth) mnamo 2004. Barraba kiko katika Bundarra-Barraba Important Bird Area (Kiswahili: Eneo Muhimu kwa ndege wa mwitu za vijiji Bundarra na Barraba) ambayo inalinda makazi ya ndege ambayo ni nadra Anthochaera phrygia (kwa Kiingereza: Regent Honeyeater).

Barabara kuu

Barraba ni km 477 kaskazini magharibi kutoka Sydney, km 548 kusini magharibi kutoka Brisbane, na km 90 kaskazini kutoka Tamworth, ambao ni mji karibu zaidi. Mto wa Manilla unapita kando ya kijiji. Barraba kiko kwenye barabara ya watalii Fossickers Way (Kiswahili: Njia ya Watafutaji wa metali ya thamani na mawe za dhamana) na kijiji kiko kwenye Nandewar Range (Kiswahili: Milima ya Nandewar) kwa urefu wa m 500.

Anthochaera phrygia

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Waaustralia wa asili, watu wa Kamilaroi (au watu wa Gamilaraay), waliishi katika wilaya hiyo kabla ya kuwasili kwa Wazungu.[2] Mzungu wa kwanza katika wilaya hiyo alikuwa mchunguzi na mtaalam wa mimea Allan Cunningham ambaye alifika huko mnamo 1827.[3] Shamba la kwanza wilayani lilianzishwa mnamo 1837 au 1838.[2][4] Tovuti ya kijiji cha baadaye iliauliwa mnamo 1852.[5]

Ugunduzi wa dhahabu katika miaka ya 1850 ulisaidia makazi kukua. Ofisi ya posta ya kwanza ilifunguliwa mnamo 1856[6] na shule ya kwanza ilifunguliwa mnamo 1861. Kanisa la Anglikana la kwanza lilijengwa mnamo 1876 na benki ya kwanza pia ilifunguliwa mnamo 1876. Hoteli ya kwanza, Commercial Hotel, ilijengwa mnamo 1878 na mahakama ilijengwa mnamo 1885. Barraba ilitangazwa rasmi kuwa kijiji mnamo 1885. Hospitali ilijengwa mnamo 1891 na kanisa la Methodisti lilijengwa mnamo 1898.

Gazeti la hapa, The Barraba Gazette, lilianza kuchapisha mnamo 1901. Reli ilifika kijijini mnamo 1908[7] lakini treni ya mwisho iliendesha mnamo 1983 na reli ilifungwa mnamo 1987.[8] Bwawa la Connors Creek lilijengwa mnamo 1933[4] ili kuboresha usambazaji wa maji kwa kijiji.

Allan Cunningham

Uchimbaji madini

[hariri | hariri chanzo]

Shaba iligunduliwa huko Gulf Creek mnamo 1889 na mgodi wa kwanza ulianzishwa mnamo 1892.[2] Gulf Creek ni kilomita 22 kaskazini mashariki kutoka kijiji Barraba. Kijiji kidogo kilianzishwa ambacho kilikuwa na hoteli, shule na ofisi ya posta.[9] Mgodi huo ulikuwa mgodi mkubwa wa shaba huko New South Wales mnamo 1901 lakini ilifungwa miaka ya 1930. Kijiji kidogo kilikuwa na wenyeji 300 mnamo 1901. Ofisi ya posta ilifunguliwa mnamo 1897 lakini ilifungwa mnamo 1966.[6] Kijiji kidogo kilitengwa.

Asbesto ilichimbwa tangu 1919 mpaka 1983 huko Woodsreef, ambayo ilikuwa kijiji kidogo kilomita 15 mashariki kutoka Barraba. Mgodi huo uliongezeka mnamo 1974. Mgodi ulizalisha tani 500,000 za asbestosi nyeupe.

Mgodi ulioachwa uliacha tani 75,000,000 za mawe ya taka na tani 25,000,000 za asbesto. Rundo la asbestosi linafunika hekta 43 na ni hadi mita 70 kwa urefu.[10]

Ripoti ya habari ya runinga mnamo 2008 ilielezea wasiwasi unaokua kwamba asbestosi itakuwa hatari kwa kiafya kwa wenyeji na wageni.[11] The Foundation for Asbestos Diseases of Australia (Kiswahili: Wakfu wa Ugonjwa wa Asbestosi wa Australia) ulidai kwamba tovuti ya mgodi lazima iboreshewe. Wakfu pia ulidai kwamba umma marufuku kuingia kwenye tovuti ya mgodi. Barabara yenye uchafu wa umma ilipitia tovuti ya mgodi hadi barabara hiyo ilifungwa mnamo 2013. Kijiji kidogo kilitengwa.

Wizara ya afya ya serikali Hunter-New England Health ilifanya uchunguzi wa kina juu ya athari za kiafya kwa jamii lakini matokeo ya uchunguzi wa kiwa huo bado hayajachapishwa.[12]

Mgodi uliyotengwa huko Woodsreef

Diatomite

[hariri | hariri chanzo]

Mgodi wa diatomite ulianzishwa mnamo 1982. Madini hii hutumiwa kutengeneza milipuko, dawa za kuulia wadudu, katika kilimo, na ujenzi.

Madini ya thamani na vito

[hariri | hariri chanzo]

Pyrite, garnet, jaspi, na shondo hupatikana wilayani. Mtu anaweza pia kupata visukuku.

Mashamba katika wilaya yana ng'ombe kwa nyama, kondoo kwa nyama na ugoya, au ngano.

Tabianchi

[hariri | hariri chanzo]

Majira ya joto ni ya joto na ya mvua. Majira ya baridi ni baridi na kavu. Joto la juu kabisa lililorekodiwa ni 41.8 ° C na joto la chini kabisa lililorekodiwa ni -9.4° C. Mvua ya wastani ya mwaka ni milimita 688.7 na mvua nzito zaidi iliyorekodiwa katika siku moja ni 194.3 mm ambayo ilinyesha tarehe 25 Februari 1955. [13]

Usambazaji wa maji

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ujenzi wa Lambo la Split Rock, wenyeji wa kijiji hicho walichota maji kutoka Mto wa Manilla, kutoka Barraba Creek, na kutoka Lambo la Conors Creek. Wakati vyanzo vya maji vilikuwa chini, wenyeji walipata maji kutoka visima vya dharura.[14][15]

Lambo la Split Rock lilijengwa mnamo 1988 na bomba kutoka lambo kwenda kijiji lilijengwa mnamo 2015.

  1. "2016 Census QuickStats – Barraba (State Suburb)". Australian Bureau of Statistics. 6 Julai 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-18. Iliwekwa mnamo 18 Agosti 2018.
  2. 2.0 2.1 2.2 "Barraba", Sydney Morning Herald Traveller, 13 Novemba 2008. Retrieved on 14 Novemba 2011. 
  3. "Barraba". Visit Tamworth. Tamworth Regional Council. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-10-15. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2011.
  4. 4.0 4.1 "Barraba Dateline". Barraba NSW – The Community Website. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 17 Machi 2012. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2011. {{cite web}}: Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  5. Boileau, Joanna (Februari 2007). "Thematic History of Nundle, Manilla and Barraba". Tamworth Regional Council. ku. 124–125. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-05. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2011.
  6. 6.0 6.1 "Post Office History". Post Office List – NSW. Premier Postal Auctions. Iliwekwa mnamo 14 Novemba 2011.
  7. "THE BARRABA RAILWAY.", National Library of Australia, 22 Septemba 1908, p. 7. Retrieved on 15 Novemba 2011. 
  8. Bozier, Rolfe. "Barraba Branch". NSWrail.net. Iliwekwa mnamo 15 Novemba 2011.
  9. "MINING IN NEW SOUTH WALES.", National Library of Australia, 29 Julai 1901, p. 8. Retrieved on 15 Novemba 2011. 
  10. Woodsreef Asbestos Mine Site Rehabilitation Private Members Statement, 29 August 2008. Archived Aprili 3, 2011, at the Wayback Machine
  11. Abandoned asbestos mine causes community outrage
  12. Woodsreef health report under wraps Archived Julai 6, 2011, at the Wayback Machine
  13. "Climate Statistics for Barraba Post Office". Climate statistics for Australian locations. Bureau of Meteorology. Iliwekwa mnamo 16 Novemba 2011.
  14. Barraba Water Supply Archived 2011-06-28 at the Wayback Machine
  15. Barraba's water supply critical

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]