[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Anguilla

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Anguilla
Ramani ya Anguilla
Mahali pa Anguilla

Anguilla ni kisiwa cha Antili Ndogo katika Karibi na pamoja na visiwa vidogo vya jirani visivyo na wakazi ni eneo la ng'ambo la Uingereza.

Kisiwa kikubwa cha Anguilla kina urefu wa km 25 na upana wa km 3; eneo lake ni km² 103 na idadi ya wakazi mnamo watu 13,500. Kipo upande wa mashariki wa Puerto Rico na upande wa kaskazini wa Saint-Martin.

Anguilla iliwahi kuwa sehemu ya Saint Kitts na Nevis ikajitenga mwaka 1980 na kubaki sehemu ya Uingereza wakati visiwa hivyo vingine vilipopata uhuru.

Jina ni neno la Kihispania kwa samaki ya mkunga kutokana na umbo lake kuwa refu na jembamba.

Uchumi wa kisiwa hutegemea hasa uvuvi na utalii.

Watu wa Angulilla wana asili ya watumwa kutoka Afrika.

Lugha ni Kiingereza.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:


Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Anguilla kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.