[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Chris Brown (mwimbaji)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Chris Brown
Brown performing at the Brisbane Entertainment Centre
Brown performing at the Brisbane Entertainment Centre
Maelezo ya awali
Amezaliwa Mei 5 1989 (1989-05-05) (umri 35)
Asili yake Tappahannock, Virginia,
United States
Aina ya muziki Pop, R&B, hip hop, dance
Kazi yake Mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, dancer, mwigizaji
Aina ya sauti Tenor
Miaka ya kazi 2005 mpaka sasa
Studio Jive, Zomba, LBW
Tovuti www.chrisbrownworld.com

Christopher Maurice "Chris" Brown (amezaliwa 5 Mei 1989) ni msanii anayerekodi muziki na mwigizaji filamu kutoka Marekani.

Alirekodi albamu yake ya kwanza akiwa na umri wa miaka 16 mwishoni mwa mwaka wa 2005 akaiita Chris Brown. Albamu hii ilihusisha wimbo wake wa kwanza "Run It!", ambao uliongoza kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri, na kumfanya msanii wa kwanza wa kiume tangu Montell Jordan kuwa na wimbo wake ukiongoza kwenye chati.[1] Albamu hii imeuza zaidi ya nakala milioni mbili katika Marekani na imethibitishwa kuhitimu kiwango cha platinamu kwa mara mbili na shirika la Recording Industry Association la Marekani (RIAA).[2]

Albamu ya pili ya Brown Exclusive, ilitolewa duniani kote Novemba 2007. Albamu hii ilitoa ngoma mbili zilizofanikiwa; wimbo wake wa pili kuwa namba moja Marekani, "Kiss Kiss" akimshirikisha T-Pain na "With You", ambao ulikuwa namba mbili kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri.[3][4], Brown imetoa toleo jipya la albamu hii liitwalo The Forever Edition. Wimbo wa kwanza katika albamu hii, "Forever", ulitolewa Mei 2008 na ulifikia namba mbili kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri.[5] Albamu ya Exclusive imethibitishwa kuhitimu kiwango cha Platinamu na shirika la RIAA.[2]

Mbali na mafanikio ya nyimbo zake pekee, Brown ameshiriki katika ngoma kadhaa kama vile "No Air", alioshirikiana na mwimbaji Jordin Sparks, "shorti like Mine" akishirikiana na rapa Bow Wow na "shawty Get Loose" akishirikiana na Lil Mama na T -Pain. Nyimbo hizi zimenyakua nafasi za tatu, kumi na tisa mtawalia katika Bango la nyimbo 100 mashuhuri.[6][7][8] Kutokana na mitindo yake ya kucheza ngoma, Brown amekuwa akilinganishwa na wasanii mashuhuri wa R & B kama vile Usher na Michael Jackson, wote ambao wamesemekana kuathiri muziki wake pakubwa.[9] Mnano mwaka wa 2009, Brown alikubali mashtaka ya kushambulia mwimbaji Rihanna, na alihukumiwa miaka mitano ya majaribio na miezi sita ya huduma kwa jamii.

Maisha na kazi

[hariri | hariri chanzo]

1988-2004: Maisha ya awali na Mwanzo wa kazi

[hariri | hariri chanzo]

Christopher Maurice Brown alizaliwa 5 Mei 1989,[10] katika mji mdogo wa Tappahannock, Virginia na Joyce Hawkins, aliyekuwa mkurugenzi wa kituo cha kuwachunga watoto, na Clinton Brown, afisa wa ukusanyaji katika gereza la hapo mtaani.[11][12] Yeye ni kitinda mimba, na ana dada mkubwa anayefanya kazi katika benki.[11] Tangu utoto mwake,Brown alikuwa anapenda muziki, ingawa hakuna mtu katika familia yake aliyehusiana na muziki; yeye alikuwa akisikiliza Albamu za muziki wa 'soul' zilizokuwa za wazazi wake,[12] lakini hatimaye, Brown alianza kupendelea muziki wa hip-hop.[10]

Brown alijifunza kuimba na kucheza akiwa na umri mdogo, mara nyingi akimtaja Michael Jackson kama mwimbaji aliyemtia moyo.[11] Kisha alianza kuimba katika kwaya ya kanisa lake na katika maonyesho kadhaa ya kuonyesha talanta mtaani.[13][14] Wakati mmoja alipokuwa akiiga wimbo wa Usher, mama yake walitambua talanta yake na wakaanza kutafuta fursa ya rekodi. [13] Wakati uo huo, Brown alikuwa amepitia mambo kadhaa binafsi. Ndoa ya wazazi wake ilikuwa tayari imevunjika, na alisema mpenzi wa mama yake alimwogofya kila wakati, kutokana na dhuluma mama yake aliyovumilia kutoka kwa mpenzi huyo.[15]

Akiwa na umri wa miaka 13, Brown alichukuliwa na kikundi kilichohusika na utayarishaji wa muziki kutoka mtaani kilipotembelea kituo cha baba yake cha kuuzia gesi kikitafuta talanta mpya.[16] Kisha mwimbaji huyu, alihamia New York. [11] Katika mwaka wa 2004, Tina Davis-aliyekuwa mkuu wa A & R katika kampuni ya utayarishaji ya Def Jam Recordings-alimgundua wakati Brown alikuwa anafanya kazi na baadhi ya wazalishaji wa mtaa. Bi. Tina alipendezwa na Brown pamoja na sauti yake wakati alipokuwa akifanyiwa majaribio ya sauti katika ofisi yake huko Island Def Jam Records mjini New York. Bila kusita, alimpeleka kukutana na mkuu wa zamani wa Island Def Jam Music Group Antonio "LA"Reid, ambaye alimchukua Brown siku hiyohiyo. "Mimi nilijua kwamba Chris alikuwa na kipawa," alisema Davis. "Na nilitaka kuwa sehemu ya uvumbuzi wa kipawa hiki." [17]

Mazungumzo na Def Jam yalidumu kwa miezi miwili, hadi Davis alipopoteza kazi yake kutokana na uunganishi wa kampuni. Kisha Brown alimwomba akuwe meneja wake. Davis alikubali, na akaanza "kukuza" mwimbaji huyu kwa kampuni kama vile Jive Records, J-Records na Warner Bros Records. Brown hatimaye alichagua kampuni ya Jive, kutokana na mafanikio yake ya kuwakuza waimbaji wachanga kama vile Britney Spears na Justin Timberlake. Brown anadai, "Mimi nilichagua kampuni ya Jive kwa sababu walikuwa na mafanikio bora katika kuwakuza wasanii wachanga katika soko la 'pop', [...] Mimi nilijua kuwa ningewateka watazamaji Wamarekani wenye asili ya Kiafrika kama mimi, lakini kampuni ya Jive ilikuwa na msingi mwema katika eneo la 'pop' na vilevile ilikuwa imefanya kazi kwa muda mrefu.[17]

2005-2006: Albamu ya kwanza na usafiri

[hariri | hariri chanzo]
Brown akitumbuiza katika hafla ya KISS 106.1 Seattle Jingle Bell Bash 8

Baada ya kusainiwa kwa kampuni ya Jive Records katika mwaka wa 2004, Brown alianza kurekodi katika mwezi wa Februari 2005. Kufikia mwezi wa Mei, kulikuwa na nyimbo 50 zilizokuwa tayari zimerekodiwa, 14 kati yazo ziliteuliwa kuwa katika orodha ya mwisho.[11] Mwimbaji huyu alifanya kazi na watayarishaji na waandishi wa nyimbo kadhaa -Scott Storch, Cool & Dre na Jazze Pha na wengineo- na kutoa maoni kwamba wao "kwa kweli walikiona kipawa [chake]".[17] Brown pia alitoa mchango kwenye albamu hiyo, na kupokea pongezi za kushiriki katika uandishi wa nyimbo tano.[11] "Mimi huandika kuhusu mambo ambayo vijana wa miaka 16 hupitia kila siku," Brown anasema. "Kwa mfano umeingia mashakani kwa sababu ya kumwingiza msichana ndani ya nyumba bila ruhusa, au huna gari la kwendesha, hivyo basi unaiba au kitu kama hicho." [18] Albamu nzima ilichukua chini ya wiki nane kutayarisha,[18] na ikatolewa 29 Novemba 2005.[19] Albamu aliyoipa jina lake Chris Brown, ilichukua nafasi ya pili kwenyeBango la nyimbo 200 mashuhuri na kuuza nakala 154,000 katika wiki yake ya kwanza.[20] Albamu ya Chris Brown ilikuwa na mafanikio kwa wakati huo; iliuza zaidi ya nakala milioni mbili katika Marekani-ambako ilithibitishwa kuhitimu kiwango cha platinumu kwa mara mbili na shirika la RIAA- na nakala milioni tatu duniani kote.[21][22] Wimbo wa kwanza wa albamu hiyo, "Run It!", ulimfanya Brown kuwa mwimbaji wa kwanza mwanamume kwanza (tangu Montell Jordan katika 1995) kuwa na wimbo wake wa kwanza ukifikia kilele cha Bango la nyimbo 100 mashuhuri-na ulibaki pale kwa muda wa wiki nne zaidi.[10] Nyimbo zingine tatu -"Yo (Excuse Me Miss)," "Gimme That" na "Say Goodbye"-zilichukua nafasi miongoni mwa nyimbo ishirini za kwanza katika chati hiyo.[23]

Mnamo 13 Juni 2006, Brown ilitoa kanda ya video iliyoitwa, safari ya Chris Brown, na iliyoonyesha video zake akisafiri nchini Uingereza na Ujapani, akijitayarisha kwa ziara yake ya kwanza ya shindano la Grammy Awards, akitayarisha video za muziki wake na blopa.

Mnamo 17 Agosti 2006 ili kukuza albamu yake zaidi, Brown alianza ziara yake kuu ya ushirikiano, iliyoitwa The Up Close na Personal Tour. Kutokana na ziara hii, utayarishaji wa albamu yake iliyofuata ulisukumwa nyuma kwa miezi miwili. Hospitali ya utafiti ya watoto ya St Jude ilipokea dola 50,000 kutoka kwa mauzo ya tiketi za safari ya Brown ya "Up Close & Personal" ya 2006. Brown pia aliimba mwanzoni mwa onyesho la mwimbaji wa R & B, Beyoncé katika safari yake ya Australia iliyoitwa The Beyoncé Experience tour.

2007-2008: Mwanzo wa Uigizaji na Albamu ya Exclusive

[hariri | hariri chanzo]

Brown amehudhuria kipindi cha UPN cha One on One na katika tukio la majaribio la kipindi cha The N' s Brandon T. Jackson Show .[24][25] Aidha, Brown alipata nafasi ndogo ya kuigiza kama mmoja wa wanabendi katika msimu wa nne wa kipindi cha Fox The O. C. katika mwezi wa Januari 2007.[26] Kisha Brown akapata nafasi yake ya kwanza katika filamu Stomp the Yard, wakiwa na Ne-Yo, Meagan Good na Columbus Short katika mwezi wa Januari 2007.[27] Baadaye Brown alishiriki katika filamu ya This Christmas, igizo la drama ambalo mhusika mkuu alikuwa ni Regina King, iliyotolewa tarehe 21 Novemba 2007.[28] Mnamo 9 Julai 2007, Brown alishiriki katika sehemu ya onyesho la MTV la My Super Sweet 16 (kwa ajili ya tukio hilo, jina lilibadilishwa na kuitwa: Chris Brown: My Super 18) kuadhimisha kutimiza kwake kwa miaka kumi na nane mjini New York.[29] Brown pia aliigiza kama mhusika wa kualikwa katika filamu ya Disney ya The Suite Life of Zack & Cody kama yeye mwenyewe.[30] Brown anatarajiwa kuigiza kama mhusika mkuu katika filamu ya drama ya mpira wa kikapu Phenom. [31]

Brown akitumbuiza katika Kituo cha Burudani cha Brisbane

Muda mfupi baada ya kumaliza ziara yake katika majira ya joto na Ne-Yo, Brown alianza kushughulikia utayarishaji wa albamu yake ya pili, Exclusive, ambayo ilitolewa Novemba 2007. Albamu ilichukua nafasi ya nne kwenye Bango la nyimbo 200 mashuhuri, na kuuza nakala 294,000 katika wiki yake ya kwanza.[32] Imeuza nakala milioni 1.9 Marekani.[33]

Kulingana na habari za MTV , Brown alisema: "Mimi bado nitaendelea vivyo hivyo ili mashabiki wangu vijana waweza kuendelea kusikiliza muziki wangu, lakini nina nyimbo chache za watu wazima." Wimbo wa kwanza wa albamu hii, "Wall to Wall", ulikuwa namba 96 katika Bango la nyimbo 100 mashuhuri, kisha ukapanda na kuwa namba 79 na namba 22 katika Bango la R & B na chati ya Hip-Hop na kuwa wimbo wake uliochukua nafasi ya chini kabisa hadi kufikia sasa. Wimbo wa "Kiss Kiss", ulioshirikisha na kutayarishwa na T-Pain, ulitolewa kama wimbo wa pili. Wimbo huu ukawa na mafanikio zaidi ya ule wa "Wall To Wall," na kufikia namba moja kwenye Bango la Marekani la nyimbo 100 mashuhuri, na kuwa wimbo wa Chris wa pili kuchukua nafasi ya kwanza tangu wimbo wa "Run It!" katika mwaka wa 2005.

Mnamo 4 Desemba 2007, Brown alitoa wimbo wa tatu kutoka kwa albamu yake "Exclusive," ulioitwa "With You", na uliotayarishwa na Stargate. Wimbo huu wa "With You" ulifika namba mbili kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri na ukaingia kwenye chati katika nchi mbalimbali duniani, hivyo basi kuwa mmoja wa nyimbo za Brown zilizofanikiwa sana kufikia sasa. Wimbo huu uliingia katika orodha ya nyimbo kumi za kwanza katika nchi za New Zealand, Singapore, Kanada, Marekani, Cypern, Ayalandi, Ufaransa, Uingereza, Malaysia, na Australia.

Brown alitoa toleo lingine la albamu ya Exclusive tarehe 3 Juni 2008. Toleo hili aliliita Exclusive: The Forever Edition, na alilitoa miezi saba baada ya kutolewa kwa toleo asili. Toleo hili mpya lilikuwa na nyimbo nne mpya, ikiwa ni pamoja na wimbo wa "Forever" ambao ulifika namba mbili kwenye Bango la nyimbo 100 mashuhuri.

Katika kupigia debe albamu yake Brown alianza ziara yake ya Exclusive Holiday Concert tour, na kutembelea zaidi ya sehemu thelathini Marekani. Alianza ziara hiyo katika eneo la Cincinnati, Ohio, tarehe 6 Desemba 2007 na aliihitimisha mnamo 9 Februari 2008 katika eneo la Honolulu, Hawaii. Video iliyorekodiwa ya ziara hiyo ilitolewa tarehe 3 Juni 2008 kama rekodi ya Exclusive: The Forever Edition. Yeye aliimba wimbo wa "With You" katika shindano la BET Awards '08 katika mwezi wa Juni 2008. Kisha Ciara alijiunga naye Brown ili wacheze pamoja kipande cha wimbo wa "Take You Down".

Brown, pamoja na The Game, ameshirikishwa katika albamu ya Nas ambayo bado haijapewa jina katika wimbo wa "Make the World Go Round", uliotayarishwa kwa ushirikiano wa The Game na Cool & Dre. [34] Yeye pia ameshirikishwa, wakiwa na Sean Garrett , katika wimbo wa Ludacris wa "What Them Girls Like" kutoka kwa albamu ya Theater of the Mind. Pia alishirikishwa kwenye wimbo wa tatu wa T-Pain "Freeze" kutoka kwa albamu yake mpya ya Thr33 Ringz . Brown alitajwa kama msanii mashuhuri wa 2008 na jarida la Billboard magazine.[35][36] Brown alisaidia kukuza mradi wa Math-A-Thon uliofaidi hospitali hiyo kwa kushiriki kama mwenyeji katika filamu ya kuukuza.[37] Brown alitoa wimbo wake wa "Take You Down" katika Januari 2009 nchini Uingereza na Ireland.

2009-hadi leo: GRAFFITI na kesi ya vurugu za kinyumbani

[hariri | hariri chanzo]

Tangu mwaka 2008, Brown ilianza kufanyia kazi albamu iliyokutarajiwa kutoka. Kulingana naye, atajaribu mwelekeo tofauti wa muziki kwenye albamu yake mpya ambayo, kwa sasa ina jina GRAFFITI akitumaini kuiga waimbaji wenzake wa Marekani, Prince na Michael Jackson. Yeye anasema, "Mimi ninataka kujibadilisha na kuwa tofauti. Kama mtindo wangu siku hizi, mimi sijaribu kufuata mtindo wa mijini pekee. Mimi nataka kuwa kama vile Prince na Michael [Jackson] na Stevie Wonder walivyokuwa. Wanaweza wakaingia kwenye aina yoyote ya muziki." [38] Brown alitoa wimbo wake wa kwanza kutoka kwenye albamu ya GRAFFITI unaoitwa "I Can Change Ya" tarehe 29 Septemba kama tarakimu ya kupakia, na video yake ilitolewa baadaye kwenye MTV, tarehe 27 Oktoba 2009. Brown pia alithibitisha kuwa wimbo wake utakaofuata utaitwa "Crawl", na ambao utatolewa wiki chache baada ya wimbo wake wa kwanza. Wao wametengeneza video za nyimbo zote mbili. Albamu ya GRAFFITI itafuata na kutolewa tarehe 15 Desemba 2009 .[39]

Brown alijipeleka katika Idara ya Polisi ya Los Angeles, kituo cha Wilshire, tarehe 8 Februari 2009, na alikamatwa kwa makosa ya kufanya vitisho vya jinai,[40] akiwa bado anafanyiwa uchunguzi kwa madai ya vurugu za nyumbani, kufuatia ugomvi na mwanamke ambaye hakutambuliwa. Ripoti ya polisi haikutaja jina la mwanamke aliyehusika katika tukio hilo kama ilivyo sera, lakini ripoti hiyo ilisema kwamba "yeye alikuwa amepata majeraha yaliyoonekana".[41] Hata hivyo, baadhi ya vyombo vya habari kama vile Los Angeles Times, CNN na MSNBC vilisema kuwa kuna watu waliokuwa wamemtambua mhasiriwa katika kesi hii, na kwamba alikuwa ni mpenzi wake na mwimbaji mwenzake wa muziki wa R & B, Rihanna. [42][43][44] Kufuatia kukamatwa kwake, mengi ya matangazo yake ya kibiashara yalifutiliwa mbali, muziki wake uliwacha kuchezwa katika vituo vingi vya redio, na yeye akajiondoa kutoka kwenye mitagusano na umma, ikiwa ni pamoja na mashindano ya Grammy Awards, 2009 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Justin Timberlake na Al Green. [44][45][46] Brown baadaye alitoa taarifa akisema, "Maneno hayawezi kuanza kueleza jinsi ninavyojuta na kusikitika kutokana na kilichotendeka." [47]

Mnamo tarehe 5 Machi 2009, Brown alishtakiwa kwa mashtaka ya kushambulia na kufanya vitisho vya jinai. Yeye alipelekwa kortini mnamo 6 Aprili 2009, na walikanusha shtaka moja la kufanya mashambulizi na lingine la kufanya vitisho vya jinai.[48] Tarehe 22 Juni 2009, Brown alikubali mashtaka yake na kukubali adhabu ya kufanya kazi ya jamii na miaka mitano ya majaribio rasmi. Kupata ushauri kuhusu vurugu za nyumbani pia ilikuwa sehemu ya uamuzi wa Jaji Patricia Schnegg, huko mahakamani.[49] Mashirika kadhaa yanayopinga vurugu hizi yalipinga uamuzi huo, wakisema kuwa adhabu hiyo haikuwa kali vya kutosha kwa uhalifu uliofanywa; kiwango cha ushawishi wa Brown kwa vijana pia kilijadiliwa, kwani vurugu hizi za nyumbani zinaaminika kuwa tabia ya kujifunza.[50][51] Tarehe 20 Julai 2009, Brown alitowa video ya dakika mbili katika tovuti ya YouTube ya kuomba msamaha kwa mashabiki wake na kwa Rihanna kwa sababu ya kosa hilo. Yeye alisema kuwa "alisikitishwa mno" na tukio hilo na kusema kwamba amerudia kuomba msamaha kutoka kwa Rihanna na "anakubali kosa lake ".[52][53][54] Brown alisema kuwa alitaka kuzungumza hapo awali kuhusu kesi hiyo lakini alishauriwa na wakili wake kutosema chochote hadi kesi hiyo imalizike kortini.[52][53][54] Katika mwezi wa 25 Agosti, Brown alihukumiwa miaka mitano ya majaribio, mwaka mmoja wa ushauri kuhusu vurugu za nyumbani, na miezi sita ya huduma kwa jamii; hakimu alitoa amri ya kuzuia ya hukumu miaka mitano kwa Brown, ambayo inamhitaji kukaa yadi 100 mbali na Rihanna, na yadi 10 katika matukio ya umma.[55][56][57]

Tarehe 2 Septemba 2009, Brown alizungumza kuhusu kesi hiyo ya unyanyasaji katika rekodi iliyofanywa kabla, ya mahojiano ya Larry King Live interview , ambayo ndiyo yaliyokuwa mahojiano yake ya kwanza tangu tukio hilo.[58][59][60][61] Yeye aliandamana na mama yake na wakili wake Marko Geragos, kwenye mahojiano hayo, ambapo alizungumza kuhusu maisha yake alipokuwa anakua akishuhudia vurugu za nyumbani; mama yake alikuwa akidhulumiwa na babake Brown wakambo. Brown alisema haya aliposikia maelezo kuhusu yale yaliyotokea katika usiku wa shambulio lake mwenyewe, alipomgonga Rihanna, "Nimeshtuka, kwa sababu, kwanza kabisa, mimi siko hivyo, na si ahadi kwamba nataka kuwa hivyo.[58] Mama yake Brown, Joyce Hawkins, alisema Brown "hajawahi kamwe kuwa mtu wa vurugu", na kwamba yeye haamini katika mzunguko wa vurugu. [58] Brown alielezea kuhusu uhusiano wake na Rihanna na kusema kwamba ulikuwa kama wa Romeo na Juliet wakati wa ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari kuhusu kesi hii, na kwamba ilikuwa ni vyombo vya habari vilivyowatenganisha kufuatia habari kuhusu shambulizi hilo.[61] Alisema kuwa hakuwa anakumbuka akimpiga Rihanna na aligundua tu kuwa alikuwa ashamchapa, na anaomba msamaha kwa sababu ya matendo yake usiku huo.[58][61][59][60][62] Kufuatia ukosoaji wa kusema hakuwa anakumbuka, Brown baadaye alisema katika taarifa yake, "Bila shaka ninakumbuka nini kilichotokea. Mara nyingi katika mahojiano, mama yangu alisema kuwa nilimwendea muda tu baada ya tukio hilo na kumwambia kila kitu. " Brown alisema kuwa, "bado alikuwa hakumbuki kilichotendeka [usiku] huo vyema".[59][60] Mapema katika mahojiano na Larry King Live , Brown alisema kwamba ni "jambo gumu" kwake kutazama picha maarufu iliyotolewa ya uso wa Rihanna ukiwa na majeraha, ambayo inaweza kuwa picha moja itakayomkaa akilini na kufuatana naye milele, na kwamba yeye bado anampenda.[58] "Nina uhakika tunaweza kuendelea kuwa marafiki," alisema Brown, "na mimi sijui kuhusu uhusiano wetu, lakini ninajua tu kwamba sisi tulibaki kama marafiki." Aidha, yeye alisema kuwa hahisi kwamba kazi yake imesitishwa.[61]

Diskografia

[hariri | hariri chanzo]
  • 2006: Ziara ya Up Close and Personal
  • 2007: Ziara ya The UCP Exclusive
  • 2009: Ziara ya Kushukuru Mashabiki [63]
Maonyesho ya kufungua
Televisheni
Mwaka Jina Uhusika Maelezo
2006 Christmas in Washington Chris Brown television special (Turner Network Television)
2007 The O.C. Will Tutt vipengele vitatu
2008 The Suite Life of Zack and Cody Chris Brown nyota mwalikwa
2011 Tosh.O Chris Brown mwalimu wa densi
Filamu
Mwka Jina Uhusika Maelezo
2007 Stomp the Yard Duron small role/film debut
This Christmas Michael 'Baby' Whitfield uhusika mkuu
2009 Blood Rogues Christopher
2010 Takers Jessie Attica[64] Executive Producer
2012 Think Like A Man
  1. Chris Brown - Run It!Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
  2. 2.0 2.1 "RIAA - Gold & Platinum". RIAA. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
  3. Reuters (2007-11-02). "R&B singer Chris Brown tops U.S. singles chart". Yahoo! 7 Music. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-10-20. Iliwekwa mnamo 2008-08-14. {{cite web}}: |author= has generic name (help); External link in |publisher= (help)
  4. [7] ^ Chris Brown - With You Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
  5. [8] ^ Chris Brown - Forever Chart Track. Accharts. Accessed 14 Agosti 2008.
  6. "Billboard - Updated Album Chart from the most FORUMS Music Magazine". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-05. Iliwekwa mnamo 2021-05-20.
  7. shortpages Like Mine Chart Track. Accharts. Accessed 16 Agosti 2008.
  8. Lil Mama and Chris Brown - shawty Get Loose - Music Charts. Accharts. Accessed 16 Agosti 2008.
  9. Billy Johnson, Jr. (2008-05-01). "Usher, Has Chris Brown Taken Your Spot?". Yahoo! Music. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-05-16. Iliwekwa mnamo 2008-08-16. {{cite web}}: External link in |publisher= (help)
  10. 10.0 10.1 10.2 Kellman, Andy. "Chris Brown Biography". Allmusic. Iliwekwa mnamo 2008-11-15.
  11. 11.0 11.1 11.2 11.3 11.4 11.5 "The new Michael Jackson". The Times. Times Online. 2006-02-12. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-17. Iliwekwa mnamo 2009-05-28.
  12. 12.0 12.1 "Chris Brown Biography". NME. Time Warner. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
  13. 13.0 13.1 "Chris Brown Biography". People. Time. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-10-02. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
  14. "Biography - Chris Brown". Getty Images. WireImage.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-02-18. Iliwekwa mnamo 2009-05-28.
  15. "VMA Showstopper Chris Brown Opens Up about His New Album, Past Pain and Looking Ahead in the September 2007 Issue of Giant Magazine". FindArticles. CBS Corporation. 2007-09-10. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-07-10. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
  16. "Celebrity Bios - Chris Brown". Us Weekly. Wenner Media. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-04-01. Iliwekwa mnamo 2008-10-11.
  17. 17.0 17.1 17.2 "Brown runs with it". Hearst Corporation. San Francisco Chronicle. 2006-10-01. Iliwekwa mnamo 2009-05-28.
  18. 18.0 18.1 Brandee J. Tecson. "Chris Brown". MTV Networks. MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-05. Iliwekwa mnamo 2009-05-30.
  19. Shaheem Reid (2005-10-06). "Chris Brown Dancing His 'Run It!' Straight Up The Charts". MTV Networks. MTV News. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-10-28. Iliwekwa mnamo 2009-05-30.
  20. Katie Hasty (2005-12-05). "'NOW!' Rebounds, Holds Brown From No. 1". Nielsen SoundScan. Billboard. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-25. Iliwekwa mnamo 2009-05-30. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  21. Saldanha, Evita. "Feature: Chris Brown". MTV India. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-19. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
  22. "Search Results". Recording Industry Association of America. 2006-12-18. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-24. Iliwekwa mnamo 2009-06-01.
  23. "Artist Chart History - Chris Brown - Singles". Billboard. Nielsen Business Media. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-02. Iliwekwa mnamo 2009-04-12.
  24. Brandee J. Tecson (7 Januari 2006). Chris Brown SWITCHES Over Ili Kaimu - Na Can't Get A Date Archived 28 Oktoba 2009 at the Wayback Machine. MTV. Accessed 27 Oktoba 2008.
  25. Brandon T Jackson Show The New York Times. Accessed 27 Oktoba 2008.
  26. Jayson Rodriguez (31 Agosti 2006). Chris Brown Scores Role On 'The OC,' Ready To Be 'Geeked Out All The Way' Archived 6 Julai 2009 at the Wayback Machine. MTV. Accessed 27 Oktoba 2008.
  27. Larry Carroll (3 Januari 2007). Ne-Yo, Chris Brown Open Up About Stepping Up For 'Stomp The Yard' Archived 28 Oktoba 2009 at the Wayback Machine. MTV. Accessed 27 Oktoba 2008.
  28. [60] ^ Larry Carroll (6 Februari 2007). 'Christmas' Crazy On Giving - Join Chris Brown On Holiday Flick's Set Archived 28 Oktoba 2009 at the Wayback Machine. MTV. Accessed 27 Oktoba 2008.
  29. [61] ^ My Super Sweet 16 - Chris Brown - Episode Summary Archived 6 Machi 2009 at the Wayback Machine. MTV. Accessed 27 Oktoba 2008.
  30. The Suite Life of Zack & Cody Archived 5 Julai 2009 at the Wayback Machine. Glam Media. Accessed 27 Oktoba 2008.
  31. Adler, Shawn (2007-03-21). "Movie File: Chris Brown, 'Ocean's Thirteen,' Michelle Trachtenberg & More". MTV. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-15. Iliwekwa mnamo 2009-01-26. {{cite web}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  32. Hasty, Katie (2007-11-14). "Jay-Z Leapfrogs Eagles, Britney For No. 1 Debut". Billboard. Nielsen Business Media. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-06-05. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
  33. Mitchell, Gail (2008-12-12). "Chris Brown Pairs With Rihanna, McGraw". Billboard. Nielsen Business Media. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-10-23. Iliwekwa mnamo 2009-01-12.
  34. "Game explains Chris Brown's appearance on Nas album". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-07-29. Iliwekwa mnamo 2009-11-23.
  35. "Top Artists - Billboard Year in Music 2008". Billboard. Nielsen Business Media. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-12-12. Iliwekwa mnamo 2008-12-12.
  36. Mitchell, Gail (2008-12-30). "Artist Of The Year: Chris Brown". Billboard. Nielsen Business Media, Inc. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-07-05. Iliwekwa mnamo 2009-01-09.
  37. St Jude Children's Research Hospital
  38. "Chris Brown's close Rihanna". ITV.com. 2008-06-27. Iliwekwa mnamo 2009-05-27.
  39. Nancy Dillon (2009-05-27). "Chris Brown Finally Speaks: 'I Ain't a Monster'". People. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-04. Iliwekwa mnamo 2009-05-27. {{cite web}}: Italic or bold markup not allowed in: |publisher= (help)
  40. Errico, Marcus (2009-02-08). "Chris Brown Arrested After Alleged Rihanna Assault". E! Online. E! Online. Iliwekwa mnamo 2009-02-08.
  41. "Sources: Brown's alleged victim was girlfriend Rihanna".
  42. "Brown arrested after alleged attack on Rihanna". MSNBC. 2009-02-09. Iliwekwa mnamo 2009-03-13.
  43. "Singer Chris Brown under investigation in alleged assault". Los Angeles Times. 2009-02-08. Iliwekwa mnamo 2009-03-13.
  44. 44.0 44.1 Schreffler, Laura (2009-02-08). "Chris Brown sought by police in battery investigation". Daily News. Mortimer Zuckerman. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-18. Iliwekwa mnamo 2009-02-08. {{cite web}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  45. Grossberg, Josh (2009-02-09). "Chris Brown Lowdown: Cops Continue Probe, Wrigley Halts Ads". E! Online. E! Online. Iliwekwa mnamo 2009-02-09. {{cite web}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  46. "Chris Brown and Rihanna: More fallout". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-02-13. Iliwekwa mnamo 2009-11-23.
  47. Tate, Ryan (15 Februari 2009). "Chris Brown Sorry About Rihanna Incident". Gawker. Iliwekwa mnamo 2009-03-18.
  48. "Chris Brown pleads not guilty in assault case", CNN, 2009-04-07. Retrieved on 2009-06-08. 
  49. Settlement reached in Chris Brown's alleged beating of Rihanna, Los Angeles Times, 22 Juni 2009
  50. Melago, Carrie (2009-06-24), "Chris Brown plea deal in Rihanna beating sends bad message, say domestic abuse experts", Daily News, ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-08-22, iliwekwa mnamo 2009-07-20 {{citation}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)
  51. Brown, DeNeen; Surdin, Ashley (2009-06-23), "Chris Brown Pleads Guilty to Assault", The Washington Post, iliwekwa mnamo 2009-07-20
  52. 52.0 52.1 "A Message From Chris", YouTube/Chris Brown Official Channel, 2009-07-20. Retrieved on 2009-07-20. 
  53. 53.0 53.1 "Chris Brown apologizes for Rihanna beating", MSN, 2009-07-20. Retrieved on 2009-07-20. Archived from the original on 2009-07-09. 
  54. 54.0 54.1 Rodriguez, Jayson. "Chris Brown Apologizes For Rihanna Assault In New Video", MTV, 2009-07-20. Retrieved on 2009-07-20. Archived from the original on 2010-01-09. 
  55. McCartney, Anthony. "Chris Brown sentenced in Rihanna assault case", 2009-09-25. Retrieved on 2009-09-25. 
  56. "Chris Brown sentenced for Rihanna assault", CNN, 2009-09-25. Retrieved on 2009-09-25. 
  57. "Chris Brown sentenced to community labour in Rihanna assault case", The Daily Telegraph, 2009-09-25. Retrieved on 2009-09-25. Archived from the original on 2010-09-15. 
  58. 58.0 58.1 58.2 58.3 58.4 Huggins, Amy. "Chris Brown says he still loves Rihanna", CNN, 2009-08-31. Retrieved on 2009-09-03. 
  59. 59.0 59.1 59.2 "Yes, Chris Brown remembers Rihanna beating", MSNBC, 2009-09-01. Retrieved on 2009-09-03. 
  60. 60.0 60.1 60.2 "Chris Brown Clarifies King Interview, Says He Recalls Rihanna Incident", Rolling Stone, 2009-09-01. Retrieved on 2009-09-03. Archived from the original on 2009-09-08. 
  61. 61.0 61.1 61.2 61.3 Lapowsky, Issie. "Chris Brown on 'Larry King Live': Relationship with Rihanna 'was sort of like Romeo and Juliet'", New Your Daily News, 2009-08-31. Retrieved on 2009-09-03. Archived from the original on 2009-09-06. 
  62. "Chris Brown: I Don't Remember Beating Rihanna", Us Weekly, 2009-08-31. Retrieved on 2009-09-03. Archived from the original on 2009-09-02. 
  63. http://www.billboard.com/ # / news/chris-brown-announces-fan-appreciation-tour-1004027466.story
  64. Adler, Shawn (2008-10-02). "Chris Brown Dances Around Bullets In Upcoming Film 'Bone Deep'". MTV. MTV Networks. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2010-03-02. Iliwekwa mnamo 2009-02-10.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]