Niu Briten
Mandhari
Niu Briten (ing. New Britain) ni kisiwa kikubwa kabisa katika Funguvisiwa la Bismarck la Papua Guinea Mpya .
Mlangobahari wa Vitiaz unatenganisha kisiwa na Guinea Mpya penyewe.
Eneo la kisiwa ni mnamo km2 36,520 inayolingana na ukubwa wa Taiwan. Kuna wakazi 513,926. Miji mikubwa zaidi wa Niu Briten ni Rabaul / Kokopo na Kimbe.
Niu Briten ni umbo la jina lake kwa lugha ya Tok Pisin.