[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Monako

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 08:27, 22 Januari 2024 na InternetArchiveBot (majadiliano | michango) (Rescuing 2 sources and tagging 0 as dead.) #IABot (v2.0.9.5)
(tofauti) ← Pitio lililotangulia | Toleo la sasa (tofauti) | Pitio linalofuata → (tofauti)
Principauté de Monaco
Principatu de Munegu

Utemi wa Monako
Bendera ya Monako Nembo ya Monako
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Deo Juvante
(kwa Kilatini: Kwa msaada wa Mungu)
Wimbo wa taifa: Hymne Monégasque
Lokeshen ya Monako
Mji mkuu Monaco1
43°44′ N 7°24′ E
Eneo lenye watu wengi Monte Carlo
Lugha rasmi Kifaransa2
Serikali Ufalme wenye katiba
(Utemi)
Albert II
Uhuru
Watemi wa Grimaldi kukubaliwa
na mfalme wa Ufaransa
kuwa wanajitegemea
1489
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
2.02 km² (193rd)
0.0%
Idadi ya watu
 - 2011 kadirio
 - 2008 sensa
 - Msongamano wa watu
 
36,371 (ya 217)
35,352
18,005/km² (ya 1)
Fedha Euro (EUR)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
CET (UTC+1)
CEST (UTC+2)
Intaneti TLD .mc
Kodi ya simu +377

-

1Monako ni dola-mji. 2Kiitalia hutumiwa pia na wengi



Map of Monaco

Utemi wa Monako (kwa Kifaransa: Principauté de Monaco; kwa Kimonako: Principatu de Munegu) au "Monako" kwa kifupi ni kati ya nchi ndogo kabisa duniani. Kuna nchi moja tu ndogo zaidi ambayo ni mji wa Vatikano. Hali halisi ni dola-mji ambako mji ni sawa na nchi na dola lote.

Eneo lake ni kanda nyembamba ufukoni mwa bahari ya Mediteranea tu, lenye urefu wa kilometa 4 pekee karibu na mpaka wa Ufaransa na Italia, lakini ndani ya eneo lililotwaliwa na Ufaransa mwaka 1859 kutoka Ufalme wa Sardinia.

Baada ya kupata nchi kavu mpya kutoka baharini eneo limeongezeka hekta 42 kuwa 202 au km² 2.02.

Kuna mitaa sita mjini au nchini ndiyo Monte Carlo, La Condamine, Fontvieille, Le Larvotto, Les Moneghetti na Monaco-Ville.

Hakuna nchi yenye msongamano mkubwa duniani kuliko Monako ikiwa na wakazi zaidi ya 18,000 kwa kilomita ya mraba.

Lugha inayotumika hasa ni Kifaransa ambayo ni lugha rasmi. Sehemu ya wananchi bado hutumia Kimonako ambacho ni lahaja ya lugha ya Kiliguria inayotumika katika mkoa wa Liguria (Italia Kaskazini).

Monako ina dini rasmi ambayo ni Ukristo wa Kanisa Katoliki. Wakazi Wakristo kwa jumla ni 83.2%.

Wananchi wachache, wageni wengi

[hariri | hariri chanzo]

Idadi ya wakazi ni takriban 35,000 ambao 5,070 au 16% ya wakazi wote ni wananchi na wengine wote ni wageni wanaoishi mjini. 47% ya wakazi ni Wafaransa, 16% Waitalia na wengine 21% ni raia wa mataifa 125 mbalimbali.

Nchi ya matajiri wengi

[hariri | hariri chanzo]

Monako haina kodi ya mapato. Hali hii imesababisha matajiri wengi kutoka nchi mbalimbali kuhamia nchini. Hivyo Monako ni nchi yenye asilimia kubwa ya mamilionea kulingana na idadi ya wakazi wote kuliko nchi yoyote duniani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya Monako imekuwa sawa na historia ya familia ya Grimaldi tangu mwanzo wake.

Akina Grimaldi walikuwa matajiri katika mji wa Genova (Italia) waliopaswa kukimbia nchi wakati wa vita ya wenyewe kwa wenyewe mwaka 1296 BK. Walinunua cheo cha kitemi pamoja na maeneo madogomadogo ya utawala katika Italia ya Kaskazini hadi Ufaransa Kusini.

Kati ya maeneo haya yote ni Monako pekee iliyobaki mikononi mwao tangu kuondoa mji mikononi mwa Genova mwaka 1419.

Watemi wa Grimaldi walifaulu kwa siasa yenye busara kupata kibali cha Wafalme wa Ufaransa kuwa eneo la kujitegemea bila mamlaka ya kifalme juu yao. Wakati ule palikuwapo na nchi nyingi ndogo sana za aina hiyo katika Ulaya, hasa Italia na Ujerumani.

Busara ya akina Grimaldi iliwawezesha kutunza uhuru wao katika karne zilizofuata, hasa wakijenga uhusiano mzuri mara na huyu mara na huyu kati ya majirani wakubwa.

Kati ya 1425 hadi 1641 akina Grimaldi waliweka nchi yao chini ya ulinzi wa Hispania wakiwalipa Wahispania pesa kwa kuweka kikosi cha wanajeshi katika boma la Monako. Tendo hilo lilikuwa utetezi dhidi ya wafalme wa Ufaransa ambao wakati mwingine walielekea kumeza nchi ndogo.

Baada ya kuchoka na Wahispania walifanya mapatano na Wafaransa waliolazimisha Hispania kuondoka.

Wakati wa mapinduzi ya Ufaransa mwaka 1789 utawala wa kifalme na kitemi ulifutwa kabisa Ufaransa na serikali ya mapinduzi haikuheshimu tena mapatano ya kukubali uhuru wa eneo la akina Grimaldi.

Lakini baada ya kipindi cha Napoleon Bonaparte, aliyerithi matunda ya mapinduzi, mataifa ya Ulaya kwenye mkutano wa Vienna mwaka 1815 yalipatana kurudisha hali jinsi ilivyowahi kuwa awali. Hivyo Wagrimaldi walirudi Monako wakiendelea kutawala hadi leo.

Nchi lindwa ya Ufaransa

[hariri | hariri chanzo]

Tangu 1918 Monako ni nchi lindwa ya Ufaransa yenye uhuru katika mambo ya ndani lakini kwa masharti kuhusu mambo ya nje. Ufaransa ina haki ya kutaja majina kwa ajili ya nafasi za Mkuu wa Polisi na Mwanasheria Mkuu.

Kiuchumi ni sehemu ya Ufaransa isipokuwa ina sheria zake juu ya kodi. Hivyo ni pia sehemu ya eneo la forodha la EU bila kuwa mwanachama wa EU.

Lakini Monako ni mwanachama wa UM na wa Halmashauri ya Ulaya.

Mkataba wa 1918 una kipengele cha kwamba uhuru wa nchi utakwisha kama hakutakuwa na mrithi tena wa familia ya Grimaldi atakayechukua cheo cha mtemi. Mtoto wa kupanga atakubaliwa kama mrithi.

Monako inavyoonekana kutoka hewani
Jumba la Mtemi
Monako na bandari ya Monako kutoka bahari

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Monako kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.