Thebes
25°43′14″N 32°36′37″E / 25.72056°N 32.61028°E
Thebes (kwa Kigiriki: Θῆβαι, Thēbai) ulikuwa mji katika Misri ya Kale karibu km 800 kusini mwa Bahari ya Mediteranea. Ilianza karibu na mji wa kisasa wa Luxor ikaendelea pia kwenye ukingo wa magharibi wa mto Nile ( 25.7° N 32.645° E ).
Thebai lilikuwa jina la Kigiriki, Wamisri wa Kale waliita Waset , ambayo ilikuwa pia jina la mkoa katika Misri ya juu.
Wakati wa Ufalme wa Kati, Farao Mentuhotep II alifanya Waset - Thebes kuwa mji mkuu wa Misri.
Hapo mahekalu makubwa yalijengwa au kupanuliwa ambayo yanaonekana hadi leo. Hasa mahekalu ya Karnak na Luxor hutembelewa na idadi kubwa ya watalii kutoka dunia yote.
Kwenye ukingo wa magharibi wa Mto Nile, wafalme walianza kujenga makaburi pamoja na mahekalu yao. Sehemu mashuhuri zaidi ni Bonde la Wafalme na hekalu la malkia Hatshepsut.
Thebes - Waset ilirudi kuwa mji mkuu mara kadhaa baada ya Mehutep II. Kuna uwezekano kwamba mnamo mwaka 1500 KK Thebes ilikuwa mji mkubwa zaidi duniani kwa wakati wake, ikiwa na wakazi 75,000[1]. Iliharibika wakati wa uasi dhidi ya mfalme Ptolemaio IX mnamo mwaka 84 KK; wakati wa Dola la Roma kikosi cha jeshi kilikaa katika hekalu la kale la Karnak. Mji wa Luxor ya leo ilikuwa kijiji kilichobaki kando ya hekalu la Luxor.
Marejeo
hariri- ↑ [https://web.archive.org/web/20110726164950/http://www.ianmorris.org/docs/social-development.pdf Ian Morris, "Social Development Archived 2011-07-26 at the Wayback Machine"]
Vyanzo
hariri- Gauthier, Henri. 1925-1931. Dictionnaire des noms géographiques contenus dans les textes hiéroglyphiques . Juzuu. 3 ya 7 vols. Cairo: Imprimerie de l'Institut français d'archéologie orientale du Caire. (Ilichapishwa tena Osnabrück: Otto Zeller Verlag, 1975). 75, 76.
- Polz, Daniel C. 2001. "Thebes". Katika The Oxford Encyclopedia ya Misri ya kale, iliyohaririwa na Donald Bruce Redford. Juzuu. 3 ya 3 vols. Oxford, New York, na Cairo: Chuo Kikuu cha Oxford Press na Chuo Kikuu cha Amerika huko Cairo Press. 384-388.
- Redford, Donald Bruce. 1992. "Thebes". In The Anchor Bible Dictionary, iliyohaririwa na David Noel Freedman. Juzuu. 6 ya 6 vols. New York: Doubleday. 442–443. (seti ya ujazo 6)
- Strudwick, Nigel C., & Strudwick, Helen, Thebes huko Misri: Mwongozo wa Makaburi na Mahekalu ya Luxor ya Kale . London: Jumba la Habari la Jumba la kumbukumbu la Briteni, 1999, ) / (karatasi)
Viungo vya nje
hariri- More information on ancient Thebes, a World Cultural Heritage site
- Theban Mapping Project
- [http://web.archive.org/20111026092022/http://archive.cyark.org/ancient-thebes-intro Archived 26 Oktoba 2011 at the Wayback Machine. Ramesseum/Ancient Thebes Digital Media Archive (photos, laser scans, panoramas)], data from an Egyptian Supreme Council of Antiquities/CyArk research partnership
- ICOMOS Heritage at Risk 2001/2002
Makala hii kuhusu maeneo ya Misri bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Thebes kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |