Steven Kanumba
Steven Charles Kanumba (mkoa wa Shinyanga, 8 Januari 1984 [1]katika - 7 Aprili 2012 [2]) alikuwa msanii wa maigizo na filamu kutoka Tanzania. Ni mmoja wa wasanii wa kwanza kufanya kazi nje ya nchi na kuvutia wasanii wa nje kuja kuigiza nchini Tanzania, hasa Wanigeria kama vile Mercy Johnson, Emmanuel France, Nkiru Silvanus, Ramsey Nouah [3]. Kanumba pia ameweza kuwaleta waongozaji filamu kadhaa wa Kinigeria nchini.
Steven Kanumba | |
---|---|
Hayati Steven Kanumba. | |
Amezaliwa | Steven Charles Kanumba Januari 8 1984 Shinyanga, Tanzania |
Amekufa | Aprili 7, 2012 (umri 28) Dar es Salaam, Tanzania |
Kazi yake | Muigizaji, Mtunzi, Mtayarishaji, Muongozaji |
Maisha
Baba yake alikuwa anaitwa Charles Kanumba na mama yake aliitwa Flora Mutegoa. Alikuwa ana uwezo wa kuongea lugha 3: Kiswahili, Kisukuma na Kiingereza.
Steven alianza elimu yake ya msingi katika Shule ya msingi Bugoyi na aliendelea na elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mwadui. Baadae alihamishiwa Vosa Mission Secondary School. Alijiunga na kidato cha 5 & 6 katika Shule ya Sekondari Jitegemee[4] iliyopo Dar-es-Salaam
Shughuli za uigizaji
Kanumba ameanza shughuli za kuigiza miaka mingi kwenye miaka ya 1990. Ambapo alianza kufahamika zaidi mwaka 2002 mara tu baada ya kujiunga na kundi la sanaa ya maigizo maarufu kama Kaole Sanaa Group lililopo Bagamoyo. Alijibebea umaarufu mkubwa nchini Tanzania na alikuwa kipenzi cha wengi na alikubalika karibia nchi zote za Afrika Mashariki na maziwa makuu. Aliweza kutangaza sanaa nchi za Afrika ya Magharibi ikiwemo Nigeria na pia Wanigeria walipendezewa na uigizaji wake hivyo kushirikiana pamoja naye katika filamu kadha wa kadha. Filamu ambazo aliwahi kuigiza ni Dar to Lagospamoja na She is My Sister .
Kifo
Kanumba alifariki baada ya kupata jeraha kwenye ubungo, ambapo jeraha hilo lilisabishwa baada ya kupata pigo kichwani tarehe 07/04/ 2012 [5] ILisemekana alikuwa na rafiki yake wa kike anayeitwa Elizabeth Michael anaye fahamika kama Lulu ambaye alikuwa na miaka 18 kipindi hicho. Lakini rafiki yake huyo alikanusha kuhusu kuhusika na kifo cha Kanumba.[6] Kanumba alipelekwa hospitali ya taifa Muhimbili akiwa mahututi ambapo, baada ya vipimo madktari walithibitisha kwamba kifo chake kilitokana na jeraha kwenye ubungo kumsababishia kukosa pumzi na kupoteza uhai hapo. Mnamo mwaka 2017, Lulu alituhumiwa kwa kuua bila kukusudia na alipewa adhabu ya kufungwa miaka 2.[7] Hukumu yake ilibadilishwa na kufanya huduma za kijamii aliachiwa jela baada ya kifungo cha mwaka mmoja released from jail 12/05 /2018. Msiba wake ulihudhuriwa na watu takribani 30,000 akiwepo mheshimiwa mama Salma Kikwete. Alizikwa katika makaburi ya Kinondoni.
Filmografia
Televisheni
- Jahazi
- Dira
- Zizimo
- Tufani
- Sayari
- Taswira
- Gharika
- Baragumu
Filamu
Mwaka | Jina | Maelezo |
---|---|---|
Haviliki | ||
Neno | ||
Ulingo | ||
Riziki | akiwa na Blandina Chagula | |
Sikitiko Langu | akiwa na Nuru Nassoro, Vincent Kigosi, Ally Chaowa na Mahsein Awadh | |
Dangerous Desire | akiwa na Vincent Kigosi, Nuru Nasoro and Blandina Chagula | |
She is My Sister | akiwa na Mercy Johnson, Nkiru Sylvanus na Yvonne Cherryl | |
Penina | akiwa na Mahsein Awadh, Emmanuel Myamba | |
Cross My Sin | akiwa na Mercy Johnson, Suzan Lewis | |
2007 | A Point Of No Return | akiwa na Wema Sepetu, Mahsein Awadh |
2008 | The Lost Twins | akiwa na Lucky Peter, Elizabeth Michael, Suzan Lewis |
The Stolen Will | akiwa na Eizabeth Chijumba, Immaculate Aloyce | |
Village Pastor | akiwa na Aunt Ezekiel | |
Magic House | akiwa na Nargis Mohamed, Issa Mussa | |
Oprah | akiwa na Irene Uwoya na Vincent Kigosi | |
Red Valentine | akiwa na Wema Sepetu, Jacquline Wolper | |
*Family Tears | akiwa na Elizabeth Michael, Wema Sepetu na Richard Bezednhout | |
The Movie's Director | akiwa na Mercy Johnson, Nkiru Sylvanus, Elizabeth Chijumba, Olufemi Ogdegbe | |
Fake Smile | akiwa na Aunt Ezekiel, Yobnesh Yusuph | |
Unfortunate Love | akiwa na Lisa Jensen, Aunt Ezekiel, Elizabeth Michael | |
Hero Of The Church | akiwa na Princess Sheila, Issa Musa, Juma Kilowoko | |
Saturday Morning | akiwa na Shamsa Ford, Hemed Suleiman, Issa Musa | |
Shauku | ||
Crazy Love | akiwa na Shamsa Ford, Hemed Suleiman, Issa Musa, Elizabeth Michael | |
2006 | Johari[8] | akiwa na Blandina Chagula na Vincent Kigosi) |
2006 | Dar 2 Lagos[8] | akiwa na Mercy Johnson, Nancy Okeke, Bimbo Akintola |
2010 | More Than Pain | akiwa na Lisa Jensen na Rose Ndauka |
2010 | Young Billionare | akiwa na Aunty Ezekiel na Patcho Mwamba |
2010 | "Ripple of Tears" | akiwa na Elizabeth Michael |
2010 | Uncle JJ | |
2010 | This Is It | |
2010 | Off Side | akiwa na Irene Uwoya, Vincent Kigosi NA Jacob Steven |
2010 | Payback | akiwa na Yvonne Cherryl, Yusuph Mlela |
2010 | Black Sunday | akiwa na Yvonne Cherryl, Yusuph Mlela, Hemed Suleiman) |
2010 | Young Billionare | akiwa na Aunty Ezekiel and Patcho Mwamba |
2011 | Saturday Morning | akiwa na Irene Paul na Ben Franko |
2011 | Deception | akiwa na Rose Ndauka, Patcho Mwamba, Bakari Makuka |
2011 | Devil Kingdom | akiwa na Ramsey Noah, Kajala Masanja |
2011 | The Shock | akiwa na Shazy Sadry |
2011 | Moses (filamu)Moses | akiwa na Suzan Lewis, Shazy Sadri, Ndumbangwe Misayo |
2012 | Big Daddy | |
2012 | Because of You | akiwa na Rose Ndauka na Grace Mapunda |
2012 | Ndoa Yangu | akiwa na Jacquline Wolper na Patcho Mwamba |
2013 | Love & Power | akiwa na Irene Paul na Patcho Mwamba; filamu ya mwisho ya Kanumba |
Marejeo
- ↑ https://www.imdb.com/name/nm2877261/bio
- ↑ https://www.bbc.com/news/world-africa-17662920
- ↑ https://millardayo.com/knmr/
- ↑ http://jitegemee.blogspot.com/
- ↑ Fresh revelations in Kanumba death probe - News. The Citizen. Retrieved on 2018-08-17.
- ↑ "Fresh revelations in Kanumba death probe - News". The Citizen. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-06-12. Iliwekwa mnamo 2018-08-17.
- ↑ "Tanzania actress Lulu Elizabeth slapped with two year jail term for killing bongo star Steven Kanumba". Daily Nation. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-17. Iliwekwa mnamo 13 Novemba 2017.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 8.0 8.1 Saur, Mahir; na wenz. (2010). Viewing African Cinema in the Twenty-First Century: Art Films and the Nollywood Video Revolution. Ohio University Press. uk. 86.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Steven Kanumba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |