Milima ya Ural
Kwa maana mengine ya neno hili tazama hapa
Milima ya Ural (Kirusi: Ура́льские го́ры - uralskiye gory) ni safu ya milima nchini Urusi na Kazakhstan inayoelekea kutoka kaskazini kwenda kusini kwa urefu wa kilomita 2,500.
Safu ya Ural hutazamiwa kama mpaka wa kijiografia inayotenganisha Ulaya na Asia hata kama kisiasa iko ndani ya Urusi inayohesabiwa kati ya nchi ya Ulaya.
Jiografia
haririUpande wa kusini safu ya Ural inaanza katika tambarare za Kazakhstan ikiendelea upande wa kaskazini hadi Bahari ya Aktiki. Kisiwa cha Novaya Zemlya ni sehemu ya kijiografia ya Ural.
Mlima mrefu wa Ural ni mlima Narodnaya (Poznurr, 1895 m).
Viungo vya Nje
haririWikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu maeneo ya Urusi bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Milima ya Ural kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |