Unyonyeshaji
Kunyonyesha ni ulishaji wa watoto wachanga na wadogo kwa maziwa kutoka kwenye titi la mwanamke.[1]
Wataalamu wa afya wanapendekeza kunyonyesha kuanzia saa ya kwanza ya maisha ya mtoto na kuendelea mara nyingi na kwa kadiri mtoto anavyotaka.[2][3] Katika wiki chache za kwanza za maisha watoto wanaweza kunyonya takriban kila masaa mawili hadi matatu, na muda wa unyonyaji kwa kawaida ni dakika kumi hadi kumi na tano kwa kila titi.[4] Watoto wakubwa hula kidogo mara nyingi.[5]
Akina mama wanaweza kukamua maziwa ili yaweze kutumika baadaye wakati ambapo unyonyeshaji hauwezekani.[1] Kunyonyesha kuna faida kadhaa kwa mama na mtoto, ambayo fomula ya watoto wachanga hukosa.[3][6]
Vifo vya takriban watoto 820,000 walio chini ya umri wa miaka mitano vinaweza kuzuilika duniani kila mwaka kutokana na kuongezeka kwa unyonyeshaji. [7] Kunyonyesha kunapunguza hatari ya maambukizi ya mfumo wa upumuaji na kuhara kwa mtoto, katika nchi zinazoendelea na zilizoendelea. [2] [3] Faida nyingine ni pamoja na hatari ndogo za pumu, mizio ya chakula, na kisukari aina ya 1 . [3] Kunyonyesha kunaweza pia kuboresha ukuaji wa utambuzi na kupunguza hatari ya unene wa kupindukia katika utu uzima. [2] Akina mama wanaweza kuhisi shinikizo la kunyonyesha, lakini katika dunia iliyoendelea watoto kwa ujumla hukua kawaida wanapolishwa kwa chupa na mchanganyiko wa maziwa ya kutengeneza. [8]
Manufaa kwa mama ni pamoja na kupoteza damu kidogo baada ya kujifungua, usinyaaji bora wa uterasi, na kupungua kwa mfadhaiko baada ya kujifungua. [3] Kunyonyesha huchelewesha kurudi kwa hedhi na uwezo wa kushika mimba, jambo linalojulikana kama amenorrhea ya unyonyeshaji. [3] Manufaa ya muda mrefu kwa mama ni pamoja na kupungua kwa hatari ya saratani ya matiti, ugonjwa wa moyo, na baridi yabisi. [3] [7] Kunyonyesha maziwa ya mama pia ni nafuu kuliko fomula ya watoto wachanga. [9] [10]
Mashirika ya afya, yakiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO), yanapendekeza kunyonyesha pekee kwa miezi sita. [2] [3] [11] Hii ina maana kwamba hakuna vyakula au vinywaji vingine, isipokuwa ikiwezekana vitamini D, ambavyo vitolewe kwa kawaida. [12] Baada ya kuanzishiwa vyakula katika umri wa miezi sita, mapendekezo mengine ni pamoja na kuendelea kunyonyesha hadi umri wa mwaka mmoja hadi miwili au zaidi. [2] [3] Ulimwenguni, takriban 38% ya watoto wachanga hunyonyeshwa tu katika miezi sita ya kwanza ya maisha. [2] Nchini Marekani mwaka wa 2015, 83% ya wanawake walianza kunyonyesha, lakini katika miezi 6 ni 58% tu waliokuwa bado wananyonyesha huku 25% wakinyonyesha peke yake. [13]
Hali za tiba ambazo haziruhusu kunyonyesha ni chache. [3] Akina mama wanaotumia dawa fulani za kujivinjari na matibabu hawapaswi kunyonyesha. [14] [15] Kuvuta tumbaku na kutumia kiasi kidogo cha pombe na/au kahawa si sababu za kuepuka kunyonyesha. [16] [17] [18]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Breastfeeding and Breast Milk: Condition Information". 19 Desemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 "Infant and young child feeding Fact sheet N°342". WHO. Februari 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Februari 2015. Iliwekwa mnamo 8 Februari 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 American Academy of Pediatrics Section on Breastfeeding. (Machi 2012). "Breastfeeding and the use of human milk". Pediatrics. 129 (3): e827–41. doi:10.1542/peds.2011-3552. PMID 22371471. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 5 Agosti 2015.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "How do I breastfeed? Skip sharing on social media links". 14 Aprili 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "What is weaning and how do I do it?". 19 Desemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ip S, Chung M, Raman G, Trikalinos TA, Lau J (Oktoba 2009). "A summary of the Agency for Healthcare Research and Quality's evidence report on breastfeeding in developed countries". Breastfeeding Medicine. 4 Suppl 1: S17–30. doi:10.1089/bfm.2009.0050. PMID 19827919.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 7.0 7.1 Victora CG, Bahl R, Barros AJ, França GV, Horton S, Krasevec J, Murch S, Sankar MJ, Walker N, Rollins NC (Januari 2016). "Breastfeeding in the 21st century: epidemiology, mechanisms, and lifelong effect". Lancet. 387 (10017): 475–90. doi:10.1016/s0140-6736(15)01024-7. PMID 26869575.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Lawrence, Ruth A.; Lawrence, Robert Michael (1 Januari 2011). Breastfeeding: A Guide for the Medical Profession. Elsevier Health Sciences. ku. 227–228. ISBN 978-1-4377-0788-5.
{{cite book}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Breastfeeding and the use of human milk. American Academy of Pediatrics. Work Group on Breastfeeding". Pediatrics. 100 (6): 1035–9. Desemba 1997. doi:10.1542/peds.100.6.1035. PMID 9411381. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Oktoba 2012.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "What are the benefits of breastfeeding?". 14 Aprili 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 10 Agosti 2015. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Kramer MS, Kakuma R (Agosti 2012). "Optimal duration of exclusive breastfeeding". The Cochrane Database of Systematic Reviews. 8 (8): CD003517. doi:10.1002/14651858.CD003517.pub2. PMC 7154583. PMID 22895934.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "What are the recommendations for breastfeeding?". 14 Aprili 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 14 Agosti 2015. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Results: Breastfeeding Rates". CDC (kwa American English). 1 Agosti 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Desemba 2018. Iliwekwa mnamo 9 Desemba 2018.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Breastfeeding and Medication". AAP.org (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-08-02. Iliwekwa mnamo 2020-01-12.
- ↑ "Are there any special conditions or situations in which I should not breastfeed?". NICHD. 19 Desemba 2013. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 Julai 2015. Iliwekwa mnamo 27 Julai 2015.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Breastfeeding and alcohol". NHS Choices. NHS. 2017-12-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 1 Agosti 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Breastfeeding and diet". NHS Choices. NHS. 2018-03-26. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Agosti 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Tobacco Use | Breastfeeding | CDC". www.cdc.gov. 2018-03-21. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Agosti 2016. Iliwekwa mnamo 4 Agosti 2016.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)