[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka UNEP)
Bendera ya UNEP.

Mradi wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Mazingira (kifupi: UNEP) ni mojawapo ya mashirika ya UM yaliyo chini ya madaraka ya Baraza la Kiuchumi na Kijamii, yaani ECOSOC [1].

Mradi huo una kazi ya kuanzisha na kuendeleza miradi ya kuhifadhi mazingira ya binadamu jinsi yalivyo na hatimaye kuyaboresha. Kwa kufanya hivi, UNEP inaonelea kuwa sote tuna jukumu la kuhifadhi na kuboresha mazingira kwa vizazi vijavyo.

Makao makuu yako mjini Nairobi, Kenya.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

UNEP ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 15 Desemba 1972 kupitia sheria ya ishirini na saba.

Mkurugenzi wa UNEP

[hariri | hariri chanzo]

Mkurugenzi wa UNEP anajulikana kama mkurugenzi-tekelezi (Executive Director).

Mnamo Disemba 1972 Mkanada Maurice Strong alichaguliwa mkurugenzi tekelezi wa kwanza wa UNEP hadi 1975. Mwandamizi wake alikuwa Mostafa Kamal Tolba kutoka Misri aliyeshika nafasi kwa miaka 17 hadi 1992.

Chini ya hao wakurugenzi umuhimu wa masuala ya mazingira ulianza kueleweka katika nchi nyingi, hasa baada ya mafanikio ya mapatano ya Montreal ya 1987 kuhusu hifadhi ya tabaka la ozoni kwenye angahewa.

Alifuatwa na Elizabeth Dowdeswell (1992–1998), Klaus Töpfer (1998–2006), Achim Steiner (2006–2016), Erik Solheim (2016-2018), Joyce Msuya (2018-2019) na Inger Andersen (2019–sasa).

Tangu mwaka 2018 kaimu mkurugenzi tekelezi ni Mtanzania Joyce Msuya.

UNEP imejihusisha na mpango wa Kyoto kupunguza gesi zinazoongeza joto duniani.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]