[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Tundra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tundra ya Aktiki kwenye Kisiwa cha Wrangel, Urusi.

Tundra ni eneo ambako miti haiwezi kustawi kutokana na halijoto duni na kipindi kifupi cha kuota kwa majani. Halijoto ya ardhi chini ya kina cha sentimita 30-200 haipandi juu ya sentigredi 0°C muda wote; hata wakati wa "joto" nI sentimita za juu pekee ambako barafu inayeyuka.

Uoto wote katika sehemu hizi ni manyasi, kuvumwani na kuvu. Kwenye ardhi ya aina hii hakuna miti, au kama iko inatokea kwa umbo la vichaka vidogo. Mpaka kati ya maeneo ya tundra na maeneo ya misitu hujulikana kama "mstari wa miti".

Kuna aina tatu za tundra:

Tabianchi katika maeneo ya tundra ni baridi kali na halijoto kidogo juu ya 0°C wakati wa wiki au miezi michache ya majira ya joto ilhali joto halitoshi kuyeyusha ardhi iliyoganda, isipokuwa kwenye sentimita za juu za ardhi.[1]

Maeneo ya Tundra duniani      Tundra karibu na ncha, penye kuvumwani na kuvu pekee (uoto unafunika 10 - 80 % za uso wa nchi)      Tundra yenye majani na vichaka vidogo (uoto unafunika zaidi ya 80 % za uso wa nchi)      Tundra ya mlimani karibu na ncha      Tundra ya mlimani ya latitudo za kati      Mbuga karibu na ncha
  1. English through Science (2010). Blue Planet. McGrawHill. {{cite book}}: Cite has empty unknown parameter: |coauthors= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tundra kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.