Rio de Janeiro
Mandhari
Rio de Janeiro ni jiji kubwa la pili nchini Brazil baada ya São Paulo.
Ilikuwa mji mkuu wa nchi hadi tarehe 21 Aprili 1960. Leo ni mji mkuu wa jimbo la shirikisho la Rio de Janeiro. Mwaka 2000 rundiko la jiji lilikuwa na wakazi 5,473,909.
Rio de Janeiro ni jiji la Brazil linalojulikana zaidi kote duniani. Ni kitovu cha utalii na cha utamaduni. Kanivali yake inavuta wageni wengi kila mwaka. Mlima wa Corcovado unabeba Sanamu ya Mwokozi ambayo ni sanamu kubwa ya Yesu yenye kimo cha mita 30.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Rio de Janeiro travel guide kutoka Wikisafiri (Kiingereza)
- Picha za Rio de Janeiro na vitongoji vyake Archived 25 Novemba 2012 at the Wayback Machine.
- Tovuti ya "City Hall" yenye takwimu mbalimbali za jiji, habari za Kanivali na sheria za manispaa (kwa Kireno).
Makala hii kuhusu maeneo ya Brazil bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Rio de Janeiro kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |