[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Dola

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Milki)

Dola (kutoka Ar. دولة daulat; nchi, serikali, taifa; ing. state) ni utaratibu wa kisiasa wa jamii katika eneo fulani.

Ufafanuzi wa "Dola"

[hariri | hariri chanzo]

Fani mbalimbali huwa na maelezo tofauti kiasi juu ya maana ya dola:

  • sheria hufundisha dola kuwa mamlaka ya jamii ya taifa; ina tabia tatu za kimsingi ambazo ni
    • eneo la dola,
    • taifa au watu wa dola na
    • mamlaka ya dola juu ya watu na eneo lake.
  • elimu jamii hufundisha kufuatana na Max Weber dola kuwa jumuiya au jamii ambayo ina mamlaka ya kukubalika ya pekee katika eneo fulani; hivyo ni uhusiano wa utawala wa watu juu ya watu unaofuata haki na sheria.
  • elimu siasa hufundisha dola kuwa muundo wa mamlaka ya umma kwa ajili ya kuratibu mambo ya umma.
  • falsafa hufundisha dola kuwa utekelezaji wa shabaha za kimaadili za kila mtu na jamii kwa pamoja; Hegel alisema dola ni mwendo wa Mungu katika historia; msingi wake ni akili inayotaka kuwa uhalisia.

Aina za Dola

[hariri | hariri chanzo]

Dola hutokea kwa maumbo mbalimbali kwa mfano jamhuri au ufalme. Dola inaweza kujitegemea kabisa au kuwa sehemu ya shirikisho au muungano kama Muungano wa Madola ya Amerika. Ndani ya maumbo haya kuna njia mbalimbali za kutekeleza mamlaka na kuratibu serikali kwa mfano kwa njia ya demokrasia au udikteta.

Vyombo vya Dola

[hariri | hariri chanzo]

Kiini cha dola ni utekelezaji wa mamlaka katika eneo fulani. Hapo kuna chombo kinachoitwa serikali chenye mamlaka haya mkononi. Serikali inaangaliwa na taasisi nyingine.

Katika madola ya kisasa kuna mgawanyo wa madaraka wa dola kwa taasisi mbalimbali:

  • bunge huamua juu ya sheria
  • serikali inatekeleza sheria
  • mahakama zinaangalia utekelezaji na kuamua kama kuna mawazo tofauti

VYombo vingine ni matawi mbalimbali ya serikali kulingana na katiba ya dola.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]