[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Sankt Peterburg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Leningrad)
Kanisa la Watakatifu Petro na Paulo mjini Peterburg

Sankt-Peterburg (Kirusi: Санкт-Петербург; majina ya kihistoria: Sankt Petersburg, St. Petersburg, Petrograd, Leningrad) ni mji mkubwa katika Urusi ya magharibi kwenye mwambao wa Bahari ya Baltiki. Kuna wakazi milioni 4.7 ikiwa ni mji mkubwa wa pili wa Urusi. Iliwahi kuwa mji mkuu wa nchi.

Sankt Peterburg ilianzishwa mwaka 1703 na Kaisari Peter I wa Urusi kama mji mkuu wake badala ya Moscow ikaendelea kama mji wa kwanza hadi 1918 wakati mji mkuu ulirudishwa Moscow baada ya mapinduzi ya kikomunisti.

Sankt Peterburg ilibadilisha jina mara kadhaa. Mwanzoni kabisa jina la Kiholanzi lilikuwa kawaida "Sankt-Pieterburch". Baadaye mji ulipewa jina lenye umbo la Kijerumani "Sankt Petersburg". Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia serikali ya Urusi ilisikitika jina ni Kijerumani hivyo likabadilihswa kuwa "Petrograd". Baada ya kifo cha Vladimir Lenin kiongozi wa mapinduzi ya Urusi mji ukapewa jina la "Leningrad" kwa heshima yake.

1991 baada ya mwisho wa Umoja wa Kisovyeti jina lilibadilishwa tena kwa kura ya wananchi kuwa "Sankt Peterburg".

Mji unapendeza sana ukiwa na nyumba nyingi za kihistoria. Mji una mifereji mingi ndani ya eneo lake hivyo huitwa pia "Venezia ya Kaskazini". Maonyesho ya sanaa yasifiwa kote duniani.

Ramani ya kale ya St Petersburg na Kronstadt.
Wikimedia Commons ina media kuhusu: