[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Kitabu cha Tobiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tobiti na Anna. Mchoro wa Abraham De Pape (1658 hivi), National Gallery of London.

Kitabu cha Tobiti ni kimojawapo kati ya vitabu vya deuterokanoni vya Biblia ya Kikristo.

Nakala zilizopatikana katika mapango ya jumuia ya Waeseni huko Qumran zinaonyesha kuwa kitabu hicho kiliandikwa kwanza kwa Kiaramu miaka 200 KK hivi na kutafsiriwa mapema kwa Kigiriki katika Septuaginta.

Inaonekana kuwa tafsiri ya Kilatini maarufu kwa jina la Vulgata iliyofanywa na Jeromu inategemea andiko asili.

Kitabu hicho kilikubaliwa kama sehemu ya Biblia na mtaguso wa Hippo (393), mtaguso wa Carthago wa mwaka 397 na wa mwaka 419, halafu tena na Mtaguso wa Florence (1442) na Mtaguso wa Trento (1546)[1][2][3][4][5][6].

Lakini hakikubaliwi na Wayahudi katika Tanakh, wala na Waprotestanti wengi.

Hadithi hiyo inahusu familia ya kabila la Naftali la taifa la Israeli katika karne ya 7 KK, baada ya uhamisho uliosababishwa na Waashuru.

Lengo lake kuu ni kufundisha maadili bora ya Wayahudi

Kama vitabu vyote vya Biblia, hiki pia kinatakiwa kisomwe katika mfululizo wa historia ya wokovu ili kukielewa kadiri ya maendeleo ya ufunuo wa Mungu kwa binadamu.

  1. http://www.tertullian.org/decretum_eng.htm
  2. "Canon XXIV. (Greek xxvii.)", The Canons of the 217 Blessed Fathers who assembled at Carthage, Christian Classics Ethereal Library
  3. B. F. Westcott, A General Survey of the History of the Canon of the New Testament (5th ed. Edinburgh, 1881), pp. 440, 541-2.
  4. Council of Carthage (A.D. 419) Canon 24
  5. Eccumenical Council of Florence and Council of Basel Session 11—4 February 1442. ewtn. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-02-20. Iliwekwa mnamo 20 Oktoba 2016. {{cite book}}: Unknown parameter |dead-url= ignored (|url-status= suggested) (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Session IV Celebrated on the eighth day of April, 1546 under Pope Paul III". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-03-23. Iliwekwa mnamo 2018-10-25.
Vitabu vya Agano la Kale

Mwanzo * Kutoka * Walawi * Hesabu * Kumbukumbu * Yoshua * Waamuzi * Ruthu * Samueli I * Samueli II * Wafalme I * Wafalme II * Mambo ya Nyakati I * Mambo ya Nyakati II * Ezra * Nehemia * TobitiDK * YudithiDK * Esta * Wamakabayo IDK * Wamakabayo IIDK * Yobu * Zaburi * Methali * Mhubiri * Hekima DK * SiraDK * Wimbo Bora * Isaya * Yeremia * Maombolezo * BarukuDK * Ezekieli * Danieli * Hosea * Yoeli * Amosi * Obadia * Yona * Mika * Nahumu * Habakuki * Sefania * Hagai * Zekaria * Malaki

Alama ya DK inaonyesha vitabu vya deuterokanoni visivyopatikana katika matoleo yote ya Biblia.

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kitabu cha Tobiti kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.