[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Airbus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Airbus 380 ni ndege kubwa ya abiria duniani na ilianza kutumiwa na Singapore Airlines
A 330-200 Air Seychelles 2013

Airbus SAS ni kampuni kubwa ya kutengeneza eropleni katika Ulaya na moja ya makampuni makubwa duniani katika fani hii.

Kwa jumla imeajiri watu 50,000 katika nchi mbalimbali na hasa katika viwanda vyake huko Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Hispania.

Tangu mwaka 2001 Airbus imekuwa kampuni inayotengeneza ndege za kusafirisha abiria nyingi duniani. Ni hasa aina mbalimbali kama vile Airbus A300, Airbus A310 au Airbus A320. Tangu mwaka 2007 Airbus A380 ni ndege kubwa kabisa ya kubeba abiria duniani.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ya Airbus ni tokeo la harakati la kuunganisha makampuni madogo zaidi katika Ulaya kwa shabaha ya kuweza kushindana na makampuni makubwa ya kutengeneza ndege ya Marekani kama vile Boeing na McDonnell Douglas.

Chanzo cha Airbus kilikuwa maungano ya makampuni ya Kijerumani kwa upande mmoja na shirikisho la makampuni ya Kifaransa. Makampuni mengine kutoka Hispania na Uingereza yalijiunga nao na mwanzoni serikali za nchi hizi zilishika asilimia kubwa ya hisa isipokuwa Ujerumani ambako kampuni la Daimler ilishika hisa za taifa hili. Hadi mwaka 2001 Wajerumani na Wafaransa walishika kila asilimia 37.9 za hisa zote, Waingereza asiilimia 20 na Wahispania 4.2.

Baadaye washiriki wote waliungana kwa kuunda kampuni la EADS (European Aeronautic Defence and Space Company) ambayo sasa ni kampuni mama ya Airbus.

Airbus 320 ni modeli iliyotengenezwa mara nyingi na kampuni hii kuna ndege 2700 za aina hii zinazofanya kazi

Aina za ndege

[hariri | hariri chanzo]

Modeli za kiraia za Airbus

[hariri | hariri chanzo]
Aina za ndege za Airbus (kufuatana na takwimu za kampuni yenyewe)
Ndege Tabia Abiria kwa kawaida Idadi juu ya abiria Imeruka mara ya kwanza Mwisho wa utengenezaji
A300 injini 2, safu 3 za viti 228–254 361 1972-10-28 2007-03-27 (jumla ndege 561)
A310 injini 2, safu 3 za viti, badiliko la A300 187 279 1982-04-03 2007-03-27 (jumla ndege 255)
A318 injini 2, safu 2 za viti, ilifupishwa 6.17 m kutoka A320 107 117 2002-01-15
A319 injini 2, safu 2 za viti, ilifupishwa 3.77 m kutoka A320 124 156 1995-08-25
A320 injini 2, safu 2 za viti 150 180 1987-02-22
A321 injini 2, safu 2 za viti, ilirefushwa 6.94 m kutoka A320 185 220 1993-03-11
A330 injini 2, safu 3 za viti 253–295 406–440 1992-11-02
A340 injini 4, safu 3 za viti 239–380 420–440 1991-10-25 2008-09 (A340-200)
2011-11-10 (modeli zote jumla ndege 375)
A350 injini 2, safu 3 za viti 270–350 550 2014 (imepangwa)
A380 injini 4, ghorofa 2, safu 3 za viti 555 853 2005-04-27
Airbus 400 ni ndege ya usafiri wa kijeshi yenye maagizo 200 kwa nchi mbalimbali

Modeli za kijeshi

[hariri | hariri chanzo]

Airbus inatengeneza pia modeli mbalimbali za ndege za usafiri wa kijeshi. Sehemu ya hizi zinafanana na modeli za kiraia zilizibadilishwa kwa mahitaji ya kijeshi lanini nyingine zimetengenezwa hasa kwa makusudi ya kijeshi. Airbus haijengi ndege za kutuopa mabomu au ya kushambulia ndege nyingine.