Ansgar Mtakatifu
Mandhari
Mtakatifu Ansgar (Amiens, Ufaransa, labda 8 Septemba 801 – Bremen Ujerumani, 3 Februari 865) alikuwa askofu mmisionari kutoka Ufaransa.
Tangu kale ametambuliwa kuwa mtakatifu.
Sikukuu yake ni 3 Februari[1].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Ansgar alijiunga na monasteri huko Corbie.
Mwaka 826 alikwenda kuhubiri Injili nchini Denmark, ambako hakufanikisha sana, hivyo akaenda Uswidi.
Alikuwa askofu wa Hamburg, halafu akaongezewaa Bremen pia, upande wa kaskazini wa Ujerumani. Ndipo alipofariki kutokana na uchovu wa kazi zake,Pia alikuwa balozi wa Papa Gregori IV katika Denmark na Uswidi.
Alivumilia magumu mengi sana katika kazi ya uenezaji Injili, asikate tamaa.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Pryce, Mark. Literary Companion to the Festivals: A Poetic Gathering to Accompany Liturgical Celebrations of Commemorations and Festivals. Minneapolis: Fortress Press, 2003.
- Tschan, Francis J. History of the Archbishops of Hamburg-Bremen. New York: Columbia University Press, 1959.
- Wood, Ian. The Missionary Life: Saints and the Evangelisation of Europe, 400 – 1050. Great Britain: Longman, 2001.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Ansgar at Birka History of Birka Archived 9 Machi 2000 at the Wayback Machine.
- Vita Ansgari, English translation from Medieval sourcebook Archived 8 Novemba 2014 at the Wayback Machine.
- German History Forum Archived 2 Novemba 2005 at the Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |