Muujiza
Muujiza ni tukio lisiloelezeka kisayansi kufuatana na sheria za maumbile.[1]
Matukio hayo yanaweza kufikiriwa yamesababishwa ama na Mungu au miungu, hata kupitia mtu wa dini, ama na nguvu nyingine zinazohusiana na ushirikina.
Hayo ni tofauti kabisa na matukio ambayo yanapatikana kwa nadra lakini yanaweza kuelezwa kisayansi ambayo watu wengine wakiyashangaa na kuyafurahia wanayaita miujiza.
Katika Ukristo
[hariri | hariri chanzo]Wanateolojia Wakristo wanasema Mungu kwa kawaida anaacha sheria za maumbile zifuate mkondo wake, lakini anabaki huru kuziingilia anavyotaka kwa mipango yake.[2]
Injili zinasimulia baadhi ya miujiza ya Yesu. Ilikuwa mingi sana; hata hivyo Injili ya Yohane (21:25) inashuhudia kwamba michache tu imeandikwa.[3][4]
Kati ya miujiza hiyo, kuna mazinguo ya kufukuza pepo wachafu, uponyaji wa maradhi mbalimbali (homa, ukoma, safura, kupooza mkono au mwili mzima, kupinda kwa mgongo, kutokwa damu mfululizo, upofu, uziwi, ububu na vilema vingine), ufufuo wa wafu, na ushindi juu ya uasilia (kama kugeuza maji kuwa divai, kutembea juu ya maji ya ziwa, kutuliza dhoruba na kuzidisha mkate na kitoweo cha samaki).[5][6]
Kwa mamlaka yake aliyoliachia Kanisa, wafuasi wengi wa Yesu wamejulikana kama watendamiujiza, ingawa wao walimrudishia Mwenyezi Mungu sifa hiyo, wakijiona vyombo vyake tu.
Kanisa Katoliki kabla ya kumtangaza muumini mwadilifu sana aliyefariki dunia kuwa mwenye heri linadai uthibitisho wa muujiza mmoja, na kabla ya kumtangaza mtakatifu muujiza mwingine.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Miracle". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-09-02. Iliwekwa mnamo 2016-03-25.
- ↑ McLaughlin, R (Mei 2002). "Do Miracles Happen Today?". IIIM Online. Reformed Perspectives Magazine. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-04-10. Iliwekwa mnamo 2 Februari 2010.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Harris, Stephen L., Understanding the Bible. Palo Alto: Mayfield. 1985. "John" p. 302-310
- ↑ The emergence of Christian theology by Eric Francis Osborn 1993 ISBN 0-521-43078-X page 100
- ↑ Graham H. Twelftree, Jesus the Miracle Worker: A Historical and Theological Study (InterVarsity Press, 1999) page 263.
- ↑ H. Van der Loos, 1965 The Miracles of Jesus, E.J. Brill Press, Netherlands.
Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |