[go: up one dir, main page]
More Web Proxy on the site http://driver.im/Nenda kwa yaliyomo

Zebaki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa Zebaki kama jina bandia la sayari angalia Utaridi


Zebaki au Hidragiri (hydrargyrum)
Tone la zebaki
Tone la zebaki
Jina la Elementi Zebaki au Hidragiri (hydrargyrum)
Alama Hg
Namba atomia 80
Mfululizo safu Metali ya mpito
Uzani atomia 200.59
Valensi 2, 8, 18, 32, 18, 2
Densiti 13.534 g/cm³
Ugumu (Mohs) {{{ugumu}}}
Kiwango cha kuyeyuka 234.32 K (-38.83 °C)
Kiwango cha kuchemka 629.88 K (356.73 °C)
Asilimia za ganda la dunia 4*10-5 %
Hali maada kiowevu
Mengineyo kiowevu kwa hali sanifu

Zebaki (jina la kisayansi: hidragiri; Kiing. mercury) ni elementi na metali duniani. Kikemia ni elementi ya mpito yenye kifupi cha Hg na namba atomia 80 katika mfumo radidia.

Jina la kawaida "zebaki" lina asili ya Kiarabu زئبق (tamka "zibaq").

Jina la kisayansi "hidragiri" latokana na Kigiriki "ὑδράργυρος" hidragiros. Ndani yake kuna maneno mawili ya ύδωρ (hidor - maji) na Άργυρος (argiros - fedha) yaani hidragiri = "fedha ya majimaji".

Wakati mwingine jina la "zebaki" linatumiwa kutaja sayari ya kwanza kutoka kwa jua inayoitwa Utaridi kwa Kiswahili; kosa hili latokana na utafsiri kutoka Kiingereza ambako metali ya zebaki na sayari ya Utaridi wote zinaitwa "en:Mercury".

Zebaki ni elementi ya pekee pamoja na bromi inayoonekana kama kiowevu kwenye hali sanifu yaani mnamo 0 °C na shindikizo la kawaida. Rangi yake ni kifedha-nyeupe.

Ni nzito sana kiasi cha kwamba chuma kinaelea ndani yake. Kwa binadamu ni sumu. Inajiunga na metali kadhaa kama aloi menginevyo haimenyuki kirahisi.

Matumizi

[hariri | hariri chanzo]

Matumizi yake ni katika mitambo na madawa. Yajulikana kama kidole cha kipimajoto kwa sababu zebaki hupanua sambamba na kupanda kwa halijoto.

Aloi zake yatumiwa pia katika tiba ya meno kwa kujaza mashimo.

Halfau ni nyongeza katika taa zinazotakiwa kutoa mwanga mkali au katika beteri.

Makala hii kuhusu mambo ya kemia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Zebaki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.